Baraza la usalama la Umoja wa Matafia latafakari kuzizuru Sudan

  • Habari NO : 769561
  • Rejea : abna.ir
Brief

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatafakari kuzizuru Sudan na Sudan Kusini mwezi huu kushinikiza kurejea kwa mchakato wa kutafuta amani.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatafakari kuzizuru Sudan na Sudan Kusini mwezi huu kushinikiza kurejea kwa mchakato wa kutafuta amani. Balozi wa Malaysia katika Baraza hilo la usalama Ramlan bin Ibrahim amesema uamuzi wa mwisho kuhusu ziara hiyo utachukuliwa baada ya tathmini ya kiusalama na kuongeza watajaribu kuzihimiza pande zinazozana Sudan Kusini kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa ya kutafuta amani. Wanadiplomasia wamesema huenda ziara hiyo ikafanyika tarehe 15 mwezi huu. Hayo yanakuja baada ya mapigano kuzuka mwishoni mwa juma lililopita katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba. Mashirika ya kutoa misaada yameonya mzozo wa kibinadamu unaoikumba nchi hiyo huenda ukaongezeka kwa viwango vikubwa.

Mwisho wa habari/ 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky