Kiir awatimua kazini mawaziri watiifu kwa Machar Sudan

  • Habari NO : 769885
  • Rejea : abna.ir
Brief

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amewafuta kazi mawaziri sita wanaogemea upande wa mpinzani wake wa muda mrefu

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir  amewafuta kazi mawaziri sita wanaogemea upande wa mpinzani wake wa muda mrefu, Riek Machar, hatua ambayo imeongeza mvutano wa kisiasa na kuongeza kitisho cha kuzuka mapigano zaidi. Katika uamuzi huo wa jana, Kiir ameteua watu wanaofungamanishwa na tawi lililojitenga na Machar la SPLM-LO, ikiwemo nafasi ya uwaziri wa mafuta. Umoja wa Mataifa umesema kiasi watu 60,000 wameyakimbia mapigano mapya yaliyozuka kati ya wafuasi wa viongozi hao wawili wanaohasimiana katika kipindi cha wiki tatu zilizopita. Mapigano hayo yamewashitua viongozi wa kanda hiyo na nchi zenye nguvu waliosaidia kuufanikisha mchakato wa Sudan Kusini kujitenga na Sudan mwaka 2011 ambapo walitarajiwa uhuru huo ungeleta mageuzi na kumaliza miongo kadhaa ya vita na ukosefu wa usalama katika eneo hilo zima la Afrika Mashariki.

Mwisho wa habari/ 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky