Boko Haram yapata kiongozi mpya

  • Habari NO : 770037
  • Rejea : abna.ir
Brief

Kundi la kigaidi la Nigeria la Boko Haram lenye mafungamano na kundi la wanamgambo wa kundi la kigaidi la wa Dola la Kiislamu au Daesh lina kiongozi mpya ambaye ametishia kuyashambulia kwa mabomu makanisa na kuwaua wakristo.

Shirila la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kundi la kigaidi la Nigeria la Boko Haram lenye mafungamano na kundi la wanamgambo wa kundi la kigaidi la  wa Dola la Kiislamu au Daesh lina kiongozi mpya ambaye ametishia kuyashambulia kwa mabomu makanisa na kuwaua wakristo.

Kulingana na jarida la kijihadi la Al Naba, Abu Musab al Barnawi ndiye kiongozi mpya wa Boko Haram aliyepewa wadhifa wa Gavana wa jimbo la magharibi mwa Afrika wa Dola la kiislamu.

Kulingana na mahojiano yaliyochapishwa na kundi la kigaidi la Daesh ambalo linamahusiano ya karibu na Saudia arabia hapo jana, al Barnawi ambaye tangu mwezi Machi mwaka jana amekuwa msemaji wa Boko Haram amesema atasitisha mashambulizi yanayolenga misikiti na masoko ya waislamu na kudai kuna njama kutoka kwa nchi za magharibi kuigeuza kanda ya kaskazini mwa Nigeria kuwa eneo la kikiristo.

Mahojiano hayo ya Al Barnawi yanaashira kubadilika kwa mkakati wa mashambulizi yanayofanywa na Boko Haram ambao wamewauwa Waislamu wengi zaidi kuliko Wakristo nchini Nigeria kwa kuishambulia misikiti, vijiji na masoko.

Boko Haram inayomaanisha elimu ya magharibi ni haram imekuwa ikizilenga pia shule kwa mashambulizi ya mabomu na kuwateka nyara watoto mashuleni.

Kiongozi huyo mpya wa Boko Haram hasa ameyashutumu mashirika ya kutoa misaada kwa kutumia hali ya ghasia kuwapa waathiriwa vyakula na makaazi na kisha kuwashawishi kubadili dini kutoka Uislamu hadi Ukristo.

Hatma ya Abubakar Shekau ambaye amekuwa kiongozi wa kundi la Boko Haram tangu mwaka 2009 haijulikani. Shekau alionekana mara ya mwisho mwezi machi katika video akionekana mnyonge na kusema mwisho wake umefika.

Kumekuwa na fununu katika wiki za hivi karibuni kuwa Shekau aliyejeruhiwa tumboni, amepokonya wadhifa wa kuwa kiongozi wa Boko haram.

Shekau yu wapi?

Mchambuzi wa masuala ya kiusalama Ryan Cummings amesema inaashira kuwa kuna mapinduzi ya uongozi ndani ya Boko Haram dhidi ya Shekau na kundi hilo linafuata mkumbo wa makundi mengine yanayojitenga na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda na kujiunga na kundi la kigaidi la Daesh lililochini ya udhamini wa Saudia arabia na washirika wake na kuongeza serikali ya Nigeria itakuwa na kibarua cha kutathmini na kukabiliana na kundi ambalo limebadilisha mkakati wake.

Tangu kuingia madarakani mwaka jana, Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameapa kulitokomeza kundi hilo la kigaidi, Operesheni kabambe za kijeshi zimefanywa dhidi yao ambapo mamia ya watu waliokuwa wameshikwa mateka wameokolewa na kundi hilo licha ya kuwa halijatokomezwa, limesambaratika.

Chini ya uongozi wa Shekau kwa miaka saba iliyopita kundi hilo limefanya uasi mkubwa Kaskazini mwa Nigeria na kusambaa hadi katika nchi jirani na Nigeria kama Niger, Chad na Cameroon.

Mashambulizi ya magaidi hao hatari yamesababisha vifo vya watu 20,000 na kuwalaazimisha wengine milioni 2.6 kuyahama makaazi yao, hali ambayo wafanyakazi wa kutoa misaada ya kibinadamu wameitaja kuwa ni janga.

Mwisho wa habari/ 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky