Chama cha Upinzani chakamata miji muhimu katika uchaguzi wa serikali za mitaa Afrika kusini

  • Habari NO : 770044
  • Rejea : abna.ir
Brief

Chama cha upinzani nchini Afrika kusini cha Democratic Alliance kinaongoza katika miji mitatu

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Chama  cha  upinzani  nchini  Afrika  kusini  cha Democratic Alliance  kinaongoza  katika  miji  mitatu mikubwa  wakati  kura  zikiendelea  kuhesabiwa  katika uchaguzi  wa  serikali  za  mitaa na  kutoa  pigo  kubwa kwa  chama  tawala  cha  African National Congress ANC tangu  kumalizika  utawala  wa  kibaguzi  miongo  miwili iliyopita.

Chama  cha  ANC , ambacho  kilifikisha  mwisho  utawala wa  Wazungu  wachache  wakati  kilipopata  ushindi  katika uchaguzi  wa  kwanza  nchini  humo  wa  kidemokrasia mwaka  1994, hata  hivyo kinaongoza  kwa  kiasi  kikubwa kwa  jumla.

Lakini  kiko  nyuma ya  chama  DA katika  miji  ya  Pretoria, Johannesburg na  Port Elizabeth, maeneo  ambayo kiliyashirikia  kwa  kiasi  fulani  bila  kupingwa.

Hali  hiyo  inaweza  kuweka  mtazamo  mpya  wa  kisiasa kabla  ya  uchaguzi  wa  taifa  wa  mwaka  2019 , na unaweza  pia  kuwatia  hamasa  mahasimu  wa  rais Jacob Zuma  katika  chama  cha  ANC  kupambana  nae.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky