Maandamano dhidi ya serikali ya Zimbabwe yapamba moto

  • Habari NO : 770550
  • Rejea : abna.ir
Brief

Serikali ya Zimbabwe iliwekewa vikwazo na nchi za Ulaya kufuatia serikali hiyo kufukuza wazungu walio kalia mali za wazimbabwe, tangu hapo serikali hiyo imekuwa ikikubwa na upinzani mkubwa wa ndani ambao unachochewa na nchi za magharibi ili kuangusha serikali ya Mugabe.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mamia ya watu wamepeperusha bendera ya Zimbabwe na kuimba wimbo wa taifa kulalamika dhidi ya serikali. Hayo yametokea wakati wa pambano la kimataifa la mchezo wa Cricket hapo jana mjini Bulawayo. Awali  polisi waliwakamata wanachama 10 wa vuguvugu la akinamama kwaajili ya mwamko wa Zimbabwe-WOZA, walipokuwa wakiandamana mbele ya uwanja wa mpira wa Cricket katika mji huo wa pili kwa ukubwa-Bulawayo."Mugabe lazima ang'atuke" ni miongoni mwa yaliyoandikwa katika mabango yaliyobebwa na waandamanaji hao wanaolalamika pia dhidi ya sera za kiuchumi za serikali."Wakati umewadia wa kutumia kila njia iliyoko. Mmojawapo wa waandamanaji Mandla Dungeni amesema maandamano yataendelea na anaamini yataleta tija. mwanaharakati mwengine wa kike anaeijiita Rose amesema, si siri kwa yeyote kwamba serikali hii imeshindwa na ndio maana mnawaona watu hawa wote waliokusanyika wakiwa na hofu kutokana na hali namna ilivyo.

Serikali ya Zimbabwe iliwekewa vikwazo na nchi za Ulaya kufuatia serikali hiyo kufukuza wazungu walio kalia mali za wazimbabwe, tangu hapo serikali hiyo imekuwa ikikubwa na upinzani mkubwa wa ndani ambao unachochewa na nchi za magharibi ili kuangusha serikali  ya Mugabe.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky