Marekani na Urusi zakutana kujadili mgogoro wa Syria

  • Habari NO : 777040
  • Rejea : abna.ir
Brief

Marekani inaunga mkono Upande wa magaidi wenye lengo la kuiangusha serikali ya Syria na Urusi inaunga mkono upande wa serikali ya Bashar asad.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mazungumzo kati ya Marekani na Urusi yenye lengo la kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano yanayoendelea nchini Syria yameonekana kukwama baada ya mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi  hizo John Kerry na mwenzake Sergei Lavrov kushindwa kufikia makubaliano. 

Marekani inaunga mkono Upande wa magaidi wenye lengo la kuiangusha serikali ya Syria na Urusi inaunga mkono upande wa serikali ya Bashar asad.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry aliwaeleza waandishi wa habari baada ya kikao kati yake na Lavrov kilichofanyika pembezoni mwa mkutano wa kilele wa G20 unaofanyika nchini China kuwa kulikuwa bado na masuala mazito ya kufanyiwa kazi  na juhudi bado zinaendelea katika kutafuta ufumbuzi wa suala hilo. 

Kikao cha mawaziri hao kimefanyika huku kiasi cha magaidi 20 wanaodhaminiwa na Marekani wakiripotiwa kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa hii leo katika mfululizo wa mashambulizi katika maeneo mengi yanayodhibitiwa na serikali nchini Syria. Mashambulizi hayo yalilenga zaidi miji ya Tartus na Homs pamoja na Hasakeh ambayo inadhibitiwa zaidi na vikosi vya kikurdi ambayo Marekani inayatumia kufanya mashambulizi dhidi ya majeshi ya serikili.  Chombo cha habari cha serikali nchini humo kimeripoti kuwa kiasi ya raia 11 wameuawa na wengine 45 kujeruhiwa katika mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani nje kidogo ya mji wa Tartus ambako ni ngome kuu ya seikali ya Rais Bashar al- Assad.

Mwisho wa habari/ 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky