Shekhe ahukumiwa miaka 5 jela kwa kuhamasisha ugaidi Uingereza

  • Habari NO : 777551
  • Rejea : abna.ir
Brief

Mahakama moja nchini Uingereza jana ilimhukumu Anjem Choudary , imamu wa Kiislamu wa dhehebu la Answari Sunna au Wahabia wenye siasa kali ....

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mahakama  moja  nchini  Uingereza  jana  ilimhukumu Anjem Choudary , imamu wa  Kiislamu  wa dhehebu la Answari Sunna au Wahabia wenye siasa kali kwenda  jela  miaka  sita  kwa  kuwahimiza  watu kuliunga  mkono  kundi  la  kigaidi la Daesh. Waendesha  mashitaka wamesema  Choudary  alitumia  mitandao  ya  kijamii kuimarisha  uungaji  wake  mkono  kundi  la  kigaidi linalojulikana  kama Daesh  Dola  la  Kiislamu ambalo ni kundi la waislamu wa madhehebu ya Sunni lenye kupata mafunzo ya kiitikadi kutoka Saudia arabia .

Alikuwa  kwa wakati  mrefu  akichunguzwa, lakini  mara kundi  la  Daesh lilipotangazwa  kuwa  ni  kundi  la  kigaidi  na mara  alipokuwa  akielezea  kuliunga  mkono  na  kuwataka watu  wengine  wajiunge  nalo, alisema  mwendesha mashitaka,  iliwezekana  kupata  ushahidi  wa  kumfikisha mahakamani na  kumfungulia  mashitaka. Lakini waendesha  mashitaka  walikuwa  wakitafuta  kwa  muda mrefu  kuhakikisha  kwamba  mtu  huyo  anafikishwa mahakamani.

Imamu  huyo  alijipatia  umaarufu  nchini  Uingereza  na nje  ya  nchi  hiyo  baada  ya  kusifu  wapiganaji  ambao walifanya  shambulio  la  Septemba  11. Pia  alikuwa anashutumiwa  kuwa  na  mahusiano  na  makundi  kadhaa ya  kigaidi  ambao  walifanya mashambulizi  duniani.

Mwisho wa habari/ 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky