Serikali ya Iran yalalamikia kuchelewa kuondolewa vikwazo

  • Habari NO : 781647
  • Rejea : abna.ir
Brief

Marekani ililazimika kusaini makubaliano hayo kwa shingo upande baada ya kuzidiwa hoja na serikali ya Iran ambayo tangu awali haikuwa na lengo la kutengeneza makombora ya maangamizi kama ilivyodaiwa na Marekani na Israel.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mkuu wa Shirika la nguvu za Atomiki nchini Iran Ali Akbar Salehi ameonya hii leo kuwa makubaliano ya nyukilia yaliyofikiwa kati ya nchi hiyo na mataifa mengine matano makubwa duniani yanaweza yakavurugika kufuatia nchi hiyo kutoondolewaa vikwazo ilivyowekea mpaka sasa.

Ali Akbar Salehi amesema hatua ya kuondolewa kwa vikwazo vyote kama ilivyoainishwa katika makubaliano hayo bado haijatekelezwa ingawa nchi yake inatekeleza wajibu wake kwa mujibu wa mkataba huo. Mkuu huyo wa shirika la Atomiki la Iran hakutaja nchi yoyote kwa kuhusika na ucheleweshaji wa kuondolewa kwa vikwazo hivyo katika maelezo yake wakati wa mkutano mkuu wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki ingawa maafisa wengine wa serikali ya Iran wameinyooshea kidole Marekani kwa kuchelewa kuiondolea Iran vikwazo vinavyohusiana na masuala ya kifedha. Iran inalalamikia kuchelewa kuondolewa haraka vikwazo vya kimataifa vinavyohusiana na masuala ya kifedha kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa wakati wa kutiwa saini mkataba huo. Rais wa Iran Hassan Rouhani alitoa kauli inayohusiana na malalamiko hayo wiki iliyopita wakati wa mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Marekani ililazimika kusaini makubaliano hayo kwa shingo upande baada ya kuzidiwa hoja na serikali ya Iran ambayo tangu awali haikuwa na lengo la kutengeneza makombora ya maangamizi kama ilivyodaiwa na Marekani na Israel.

Mwisho wa habari/ 291

 

 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky