Italy yapitisha kanuni ya kupunguza idadi ya ujenzi wa misikiti

  • Habari NO : 782677
  • Rejea : ABNA
Brief

Viongozi wa mji wa Liguria nchini Italy wamepitisha kanuni ambayo kwa mujibu wa kanuni hiyo: kutengeza msikiti mpya katika mji huo mkubwa ni jambo lisilo wezekana, ambapo kama watataka kutengeza sehemu ya ibada lazima waruhusiwe na sekta mbalimbali sehemu hiyo kitu ambacho kinaashiria kutowezekana kwa suala hilo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kanuni ya ajabu imepitishwa katika mji wa Liguria nchini Italy inayosisitiza ugumu wa kuruhusiwa kujenga msikiti mpya katika mji huo.
Kanuni hiyo imeonekana ina upinzani mkubwa kwa kupingwa na watu wengi katika nchi hiyo wakidai kuwa kanuni hiyo inapingana na katiba ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa maelezo ya vyombo vya habari vya Italy kwamba: kanuni hiyo imepitishwa siku ya Jumatano iliopita katika bunge la mji huo wa “Liguria” ambapo ulifikishwa muswada huo hatimaye kupigiwa kura za ndio 16 na zingine 15 zikipinga muswada huyo, hatimaye kupitishwa kutokana na kuungwa mkono kanuni hiyo.
Kanuni hiyo inasema kuwa kujengwa kwa jengo lingine lolote la kidini ni lazima ipatikane ruhusa toka kwa viongozi wakuu wa mji huo, huku vyombo vya habari vya sehemu hiyo vinasisitiza kuwa: kujenga msikiti ambayo huwa ina minara katika mji huo, ni jambo halipaswi kwa maana aina ya ujenzi huo ni wakale ambapo usanifu huo hauendani na usanifu wa majengo ya Italy na jinsi ya uhandisi wake.
Aidha pamoja kuwa kanuni hiyo imepingwa na Waislamu wa nchi hiyo, pia kuna idadi kubwa ya wanasiasa wa nchi hiyo wamepinga kanuni hiyo wakisema kuwa: kanuni hiyo inakinzana  kwa wazi na katiba ya nchi hiyo.
Hii ni katika hali ambayo wanaounga mkuno kanoni hiyo wamesema wakidai kuwa: wananchi wote wanapaswa kuheshimu hali ya dhahiri ya mji huo kwani kanuni hiyo haimbani mwananchi yeyote katika mji huo.
Kanuni hiyo inamruhusu msimamizi wa mji huo kufanya uchunguzi hata katika eneo linalotakiwa kujengwa, ili aweze kuruhusu na kama hataruhusu basi hakutaruhusiwa kujengwa.
Hii ni katika hali ambayo katiba ya Italy inaruhusu wananchi wa nchi hiyo na taasisi yeyote kujenga majengo ya kidini pasina kufuata hatua hizo.
Kanuni kama hiyo ya kuzuia kujenga misikiti pia ilipitishwa katika mji wa Lombardy nchini Italy kupitia viongozi wa mji huo mwaka 2015, lakini ilipingwa na mahakama kuu ya nchi hiyo kwa dalili kuwa inapingana na haki ya uhuru wa kuabudu ya wananchi wa nchi hiyo.
mwisho wa Habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky