Ufaransa yafikisha mswada wa kutetea magaidi wa Syria, Umoja wa mataifa, Urusi yapinga

  • Habari NO : 784500
  • Rejea : abna.ir
Brief

Weledi wa mambo wanazishangaa Marekani, Ufaransa na Umoja wa mataifa kwa kuitisha kikao cha kutetea magaidi nchini Syria na kuacha kuitisha kikao cha kutetea raia wa Yemen ambao kila siku wanauawa na ndege za kivita za Saudia arabia ikishirikiana na mataifa 11 ya kiarabu na kuungwa mkono na Marekani, uingereza, Ufaransa na Israel.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: wakati serikali ya Ufaransa ikiwasilisha mswada unaowatetea na kuwapa kinga magaidi nchini Syria, Urusi yapinga vikali mswada huo. Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Urusi imesema leo kuwa rasimu  iliyowasilishwa na Ufaransa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Syria inawasaidia na kuwateta magaidi katika eneo la Aleppo kwa kuwakinga magaidi hao dhidi ya mashambulizi ya angani.

Taarifa ya wizara hiyo pia imesema rasimu hiyo ya Ufaransa iliingizwa siasa na yenye kuegemea upande mmoja. Urusi jana ilipiga kura ya turufu kupinga azimio hilo, ambalo lilitaka kukomeshwa mashambzlizi ya angani dhidi ya magaidi mjini Aleppo na kuruka ndege za kijeshi katika eneo hilo. Wakati huo huo, majeshi ya serikali ya Syria yameendelea leo na operesheni yake ya angani na nchi kavu katika juhudi za kuukomboa mji huo kutoka kwa magaidi wanaoungwa mkono na Marekani na Ulaya.

Marekani na washirika wake walikimbilia kuitisha kikao cha dharura umoja wa mataifa baada ya kuona magaidi wao wameelemewa na majeshi ya Syria.

Weledi wa mambo wanazishangaa Marekani, Ufaransa na Umoja wa mataifa kwa kuitisha kikao cha kutetea magaidi nchini Syria na kuacha kuitisha kikao cha kutetea raia wa Yemen ambao kila siku wanauawa na ndege za kivita za Saudia arabia ikishirikiana na mataifa 11 ya kiarabu na kuungwa mkono na Marekani, uingereza, Ufaransa na Israel.

Jana ndege za Saudia arabia zimeshambulia sherehe na kuua watu zaidi ya 150.

Mwisho wa habari/ 291

Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky