Kiongozi wa Katoliki aomba usitishwaji vita Syria

  • Habari NO : 785081
  • Rejea : abna.ir
Brief

Kiongozi wa kanisa la Katoliki Duniani aomba vita visitishwe Syria.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kiongozi wa kanisa la Katoliki Duniani aomba vita visitishwe Syria.

Ndege za kivita za Urusi zimerejelea mashambulizi mazito ya angani katika ngome ya magaidi wanaodhaminiwa na Marekani  Aleppo na kuua magaidi takriban 25.

Papa Francis ataka usitishwaji vita ili raia na watoto waondolewe.

Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis ameyasihi makundi yanayopigana nchini Syria kusitisha vita mara moja. Wito wa Papa unajiri kufuatia mashambulizi makali yanayofanywa na Urusi hivi sasa mjini Aleppo ambapo Marekani inaendelea kuwasaidia magaidi nchini humo.

Mashambulizi mazito ya angani ambayo yamefanywa na Urusi katika ngome za magaidi wa Marekani katika maeneo ya Aleppo ndiyo ya karibuni zaidi baada ya siku kadhaa za utulivu kufuatia tangazo la Syria wiki jana kuwa ingelipunguza mashambulizi, ili kuruhusu raia waondoke katika ngome za magaidi hao. Kulingana na kundi moja la kutetea haki za kibinadamu, magaidi 25 wameuawa. Lakini maafisa wanaotoa misaada ya waokozi wamesema zaidi ya magaidi 50 wameuawa kufuatia mashambulizi hayo ambayo yamefanywa na ndege za Urusi.

Kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis ameyasihi makundi yanayoshiriki vita nchini Syria kusitisha vita mara moja ili kuruhusu raia waondolewe. Akiwahutubia maelfu ya watu katika uwanja wa Mtakatifu Petero mjini Roma, Papa Francis amesema anatoa wito kwa viongozi kunusuru raia hasa watoto ambao wamezingiriwa katika maeneo yanayoshambiliwa. Papa Francis amesema 

"Ninataka kuangazia na nisisitize ukaribu wangu na waathiriwa wa mashambulizi ya kinyama nchini Syria. Ni kwa haja ya dharura ambapo ninarejelea wito wangu kwa nguvu zangu zote kuwasihi wanaohusika kuyasitisha mashambulizi mara moja, ili kuruhusu raia waondolewe hasa watoto ambao bado wamezingirwa katika maeneo yanayoshambuliwa".

Mashambulizi hayo yanajiri wakati jamii ya kimataifa ikikumbwa na ghadhabu kuhusu mustakabali wa raia 250,000 ambao bado wapo katika ngome za magaidi wanaoungwa mkono na marekani. Mashambulizi ambayo yanajiri baada ya Marekani kuwasaidia magaidi na kusababisha kuvunjika kwa mkataba wa usitishwaji vita ulioafikiwa kati ya Marekani  na Urusi.  Suala ambalo limezua mvutano kati ya Urusi na Ufaransa na mataifa mengine yanayounga mkono magaidi nchini Syria,  huku Marekani ikitangaza kusitisha ushirikiano wake na Urusi kuhusu masuala ya kusitisha vita Syria, nayo Ufaransa ikisema itataka Mahakama ya kimataifa kuichunguza Urusi kwa makosa ya uhalifu wa kivita. Rais wa Urusi Vladimir Putin amekatisha ziara yake iliyotarajiwa wiki kesho mjini Paris baada ya rais wa Ufaransa Francois Hollande kusema atazungumza naye tu kuhusu masuala ya Syria.

Naye waziri wa masuala ya kigeni wa Uingereza Boris Johnson ameyataka makundi ya kuteta haki za kibinadamu nchini mwake kupiga kambi nje ya afisi za ubalozi wa Urusi kama njia ya kuishinikiza Urusi kukomesha mashambulizi mjini Aleppo.

Shirika la uangalizi wa haki za kibinadamu la Syria lenye makao yake makuu London pia limeripoti kuwa magaidi wanaoungwa mkono na Marekani ikishirikiana na mataifa zaidi ya 60 wamerusha makombora katika shule moja ya msingi kusini mwa mji wa Deraa, na kuua watoto watano.

Marekani na washirika wake wamekuwa wakisaidia magaidi nchini Syria ili kuangusha serikali ya Bashar asad  kama walivyofanya kwa serikali ya Gaddafi Libya, Urusi, China na Iran zimesema hazita ruhusu Marekani na washirika wake wafanya unyama kama walioufanya Libya.

Mwisho wa habari/ 291

 

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky