Kwa mara ya kwanza Marekani na Uingereza zataka mgogoro wa Yemen umalizike

  • Habari NO : 786180
  • Rejea : abna.ir
Brief

Kwa Mara ya kwanza Marekani na Uingereza ambao ni wadhamini wakuu wa mashambulizi ya kinyama dhidi ya raia wa Yemen wametaka vita dhidi ya raia wa Yemen kusimamishwa.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kwa Mara ya kwanza Marekani na Uingereza ambao ni wadhamini wakuu wa mashambulizi ya kinyama dhidi ya raia wa Yemen wametaka vita dhidi ya raia wa Yemen kusimamishwa.

Wanadiplomasia wa ngazi za juu kutoka Marekani na Uingereza wametoa mwito wakitaka kumalizika kwa mgogoro wa Yemen ambao umedumu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry pamoja na mwenzake wa Uingereza, Boris Johnson, wamesema ni wakati sasa kusitisha mapigano pasipo masharti na kuanzisha majadiliano yenye lengo la kumaliza mapigano hayo. Mgogoro huo wa Yemen ulianza mwezi Machi mwaka jana wakati  wananchi wa Yemen walipopinga uongozi wa rais Hadi na kuanzisha mashambulizi kwa lengo la kuun'goa madarakani utawala wa Rais Abd Rabbu Mansour Hadi anayeungwa mkono na nchi za Marekani. Saudi Arabia ambayo ni mshirika wa karibu wa Marekani na Uingereza ilianzisha mashambulizi ya anga dhidi ya wananchi wanaodai demokrasia mnamo Machi 2015. Mapema mwezi huu, mashambulizi ya anga ya Saudi Arabia yaliwaua watu  700 wakati wa mazishi katika kile ambacho Saudi Arabia inasema ilikuwa ni kwa makosa.

Hata hivyo mashambulizi hayo yanayoungwa mkono na Marekani na vibaraka wake yameshindwa kufikia malengo yake  nchini humo zaidi ya kuuwa wananchi wasio na hatia, huku Umoja wa mataifa ukiwa umefumba macho na mdomo wake kuhusiana na jinai na unyama unaofanywa na vibaraka wa Marekani nchini Yemen.

Wakati hayo yakiendelea serikali ya  Emirati imetangaza kuondoa majeshi yake nchini Yemen, baada ya nchi hiyo kupata hasara kubwa katika uwanja wa vita.

Ni muhumu kuashiria kuwa nchi zaidi ya 11 zimepeleka majeshi nchini Yemen kuisaidia Saudia arabia kushambulia raia wa Yemen na kuungwa mkono na serikali za Marekani, Uingereza, Ufaransa na Israel.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky