Syria na Urusi zasitisha mashambulizi kwa muda Aleppo

  • Habari NO : 786384
  • Rejea : abna.ir
Brief

Waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu amesema ndege za kivita za Urusi na Syria zimesitisha mashambulizi yake dhidi ya magaidi wanaodhaminiwa na Marekani katika mji wa Aleppo kwa nia ya kuruhusu magidi na wanajeshi wa Marekani na washirika wake waliokuwa wanasaidia magaidi kuondoka katika mji huo baada ya kusalimu amri.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu amesema ndege za kivita za Urusi na Syria zimesitisha mashambulizi yake dhidi ya magaidi wanaodhaminiwa na Marekani katika mji wa Aleppo kwa nia ya kuruhusu magidi na wanajeshi wa Marekani na washirika wake waliokuwa wanasaidia magaidi  kuondoka katika mji huo baada ya kusalimu amri.

Waziri  wa  ulinzi   wa  Urusi  amesema   kwamba  ndege za  kivita  za  Syria  na  Urusi  zimesitisha  mashambulizi yao  ya  anga  leo  katika  mji  uliozingirwa wa  Aleppo katika  matayarisho  ya  usitishaji  wa  muda  wa  mapigano ambao  Urusi  ilitangaza  kwamba  utaanza  baadaye  wiki hii.

Kwa  mujibu  wa  waziri  wa  ulinzi  wa  Urusi  Sergei Shoigu , usitishaji  wa  mashambulizi  ya  anga  utasaidia katika  kusafisha   njia  kwa majeshi ya  magaidi na wadhamini wao kuondoka katika mji huo baada ya kuzidiwa na majeshi ya Syria, hatua hii itasababisha raia wa mji huo kupata amani tena.

Mashambulizi  ya   anga  ya  majeshi  ya  Urusi  na  Syria dhidi  ya  magaidi katika mji wa Aleppo  yamesitishwa mapema  leo  asubuhi, Shoigu  alisema , akielezea  usitishaji  huo  wa  muda kuwa  ni  matayarisho  ya  kufungua  maeneo  maalum kwa  magaidi na wanajeshi wa Marekani na washirika wake ambao wamezingirwa kuondoka  mjini  Aleppo  ifikapo  Alhamis, ambapo  Urusi  ilitangaza , usitishaji  mapigano  kwa sababu  za  kiutu  kati  ya  mbili  asubuhi  hadi  saa  kumi jioni  kwa  saa  za  Syria  kuruhusu  magaidi na wanajeshi wa Marekani wanaosaidia magaidi kupata  njia  ya kuondoka kupita  kutoka  katika  mji  huo baada ya Marekani kulazimika kusalimu amri.

Mwakilishi  maalum  wa  Urusi  katika  Umoja  wa  mataifa Vitali Churkin  ambaye  anashikilia  kwa  sasa  urais  wa baraza  la  Usalama  la  Umoja  wa  Mataifa   wa kupokezana  alitangaza  hatua  hiyo  katika  Umoja  wa Mataifa jana.

"Sisi  tumetangaza  masaa  manane   ya  kusitisha mapigano. Nadhani  kwamba  usitishaji  mrefu  zaidi  kama masaa 48  ama  72 utahitaji aina  fulani  ya  makubaliano ya  pande zote."

Katika  wakati  huo , majeshi  ya  Syria  na  Urusi yatajizuwia  kuchukua  hatua  yoyote  ya  mashambulio. Magaidi  wa  Syria , ikiwa  ni  pamoja  na  wanamgambo  wa al-Qaeda na wanajeshi wa Marekani wanaoshirikiana na magaidi hao, pamoja  na  waliojeruhiwa  na  wagonjwa wataruhusiwa  kuondoka kwenda  katika  jimbo  jirani linalodhibitiwa  na  magaidi  la  Idlib.

Ushawishi  wa  mataifa  kwa  magaidi wanaodhaminiwa na Marekani

Waziri Shoigu  ameongeza  kwamba , Urusi  inayaomba mataifa  yanayosaidia magaidi  mashariki  mwa Aleppo  kuwashawishi  viongozi  wao  kuacha  mapigano na  waondoke kutoka  mji  huo kabla haijaanzisha mashambulizi makali zaidi. Ameongeza  kwamba majeshi  ya  Syria  yatarejea  nyuma  hadi  katika   maeneo ambayo  yataruhusu  magaidi na askari wa marekani wanaosaidia magaidi kupita  bila  matatizo  kwa wale  wenye  silaha kupitia  maeneo  mawili , ikiwa  ni pamoja  na  barabara  kuu  muhimu  ya  Castello. Juhudi hizo  za  Urusi  pia  zitatoa  nafasi  bora  kwa  mazungumzo baina  ya  wataalamu  wa  kijeshi  kutoka  mataifa  mbali mbali  ambayo  yanatarajiwa  kuanza  mjini  Geneva kesho Jumatano.

Msemaji  wa  katibu  mkuu  wa  Umoja  wa  mataifa Stephane Dujarric  alisema  baada  ya  kutopatikana  hatua ya  maana  katika  mashauriano  ya  faragha  yaliyofanyika katika  baraza  la  Usalama  la  Umoja  wa  Mataifa kuhusiana  na  suala  hilo  la  Syria kwamba  kilichotakiwa ni  kupata  uwezekano  wa  kupunguza matumizi  ya nguvu.

"Upunguzaji wa  ghasia , kupunguza  mapigano, usitishaji wa  aina  yoyote  ambao  utekelezaji  wake  utakuwa muhimu  sana. Tumekuwa  tukitoa  wito  wa  usitishaji  wa masaa  48 ili  kuruhusu askari wa Marekani walikuwa hai kuondoka.

Katika  mkutano mwishoni  mwa  wiki  uliosimamiwa  kwa pamoja  na  waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Urusi Sergey Lavrov  na   John Kerry  wa  Marekani , mawaziri wa  mambo  ya  kigeni  wa  Saudi  Arabia, Uturuki  na Qatar  walisema  watafanyakazi  kuwatenganisha  makundi ya  kigaidi  yenye  msimamo  wa  wastani  mjini  Aleppo kutoka  kundi la kigaidi la al-Qaeda  katika mzozo  wa  Syria  kama  al-Nusra  Front.

Marekani na washirka wake walikuwa wakipiga kerere kuwa Urusi inaua raia katika mji wa Allepo kumbe ilikuwa inatetea wanajeshi wao walikuwa wakisaidia magaidi wasiendelee kuawa na mashambulizi makali ya Urusi.

Mwisho wa habari/ 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky