Viongozi wa Ulaya kuzijadili Ukraine na Syria

  • Habari NO : 786625
  • Rejea : abna.ir
Brief

Rais wa Urusi Vladmir Putin atakabiliana na shinikizo la mataifa ya Magahribi ambayo yanaunga mkono upande wa magaidi nchini Syria kuhusiana na migogoro ya Ukraine na Syria, katika mazungumzo yanayoandaliwa mjini Berlin, atakapouzuru mji mkuu wa Ujerumani siku ya Jumatano.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Urusi Vladmir Putin atakabiliana na shinikizo la mataifa ya Magahribi ambayo yanaunga mkono upande wa magaidi nchini Syria kuhusiana na migogoro ya Ukraine na Syria, katika mazungumzo yanayoandaliwa mjini Berlin, atakapouzuru mji mkuu wa Ujerumani siku ya Jumatano.

Mwenyeji wa mazungumzo hayo Kansela Angela Merkel alisema mazungumzo hayo ambayo yanazihusisha pia Ufaransa na Ukraine, katika mkutano wa kwanza wa pande nne baada ya kupita zaidi ya mwaka mmoja, yanalenga kutoa tathmini ya kweli kuhusu hatua zilizopigwa katika utekekezaji wa mkataba wa amani wa Minsk kwa ajili ya Ukraine.

Mkutano huu unakuja siku moja baada ya ikulu ya Kremlin kutangaza kuwa vikosi vya anga vya Urusi na Syria vimesitisha mashambulizi mjini Aleppo kufuatia Majeshi ya Marekani na magaidi kusalimu amri , hatua ambayo Moscow ilisema imeonyesha nia njema waliyo nayo. Ni tangazo lililokaribishwa na Umoja na Umoja wa Ulaya na Umoja wa Ulaya, ambao hata hivyo ulisema muda wa usitishaji ulitakiwa kuwa mrefu zaidi kuwezesha ufikishaji misaada.

Merkel alisema yeye pamoja na rais wa Ufaransa Francois Hollande wataijadili Syria na rais Putin kandoni mwa mkutano huo ambao ni makhsusi kwa ajili ya Ukraine, lakini alitahadharisha juu ya matarajio ya miujiza. Alisema hata hivyo kwamba vikwazo dhidi ya Urusi kutokana na matendo yake nchini Syria vinapwswa kuendelea kuwa njia mojawapo ya kushinikiza nchi hiyo

"Hatutarajii miujiza"

"Ni wazi kwamba katika muktadha wa mkutano kama huu, rais wa Ufaransa na mimi mwenyewe, tunatumia fursa kuzungumza na rais wa Urusi kuhusu hali nchini Syria. Tayari nimefanya hivyo kwa mapana katika mkutano wa kilele wa G20 mjini Hangzhou - na rais wa Ufaransa pia amefanya hivyo.

Hali imekuwa ya maafa zaidi zaidi, kuhusiana na hali ya kibinaadamu, na hii pia ni kwa sababu ya mashambulizi ya Syria na Urusi dhidi ya watu wasiojiweza, hospitali na madakatari," alisema Merkel.

Merkel na Hollande wamekosoa vikali uungaji mkono wa Urusi kwa vikosi vya rais wa Syria Bashar al-Assad.  Na hasira zao zimepanda pale majeshi ya Syria yalipozingira mji wa magaidi ambapo ndani yake kulikuwa na vikosi vya Marekani na washirika wake wa nchi 61 wanaounga mkono magaidi, uwepo wa wanajeshi hao kwanza ni kinyume cha sheria kwani wamevuka mipaka ya Syria bila ruhsa ya serikali pili vikosi hivyo vipo kwa ajili ya kusaidia magaidi na si kupambana na magaidi nchini Syria.

Merkel alisema pia kwamba kipaumbele kwa wakati huu ni "kwamba tuangalie uwezekano wa kupunguza mateso ya watu kwa njia fulani na kulitaja hilo kuwa suala katika mkutano huo unaofanyika Jumatano jioni. Aliyasema hayo katika mkutano wa pamoja kwa waandishi wa habari na rais wa Panama Juan Carlos Varela.

Jambo la kushangaza ni kwamba nchi hizi zimesahau kuwa wananchi wa Yemen wapo kwenye mateso makali zaidi na badala yake wakuu wa Ulaya wamejikita katika kutetea magaidi wanaouawa nchini Syria.

Vikwazo kuendelea kuzingatiwa

"Maoni yangu ni kwamba hakuna njia, ikwemo ile ya vikwazo, inaweza kuondolewa mezani kwa kuzingatia hali ilivyo Syria, lakini kipaumbele ni kwamba tuangalia namna ya kupunguza mateso ya watu kwa njia fulani. Pia katika hili hatutarajii miujiza,lakini mazungumzo ni muhimu wakati wote, hata wakati mitazamo inatofautiana sana," aliongeza kansela huyo wa Ujerumani.

Mkutano huu wa Berlin unafanyika katika mkesha wa mkutano mkuu wa kilele wa viongozi wa mazaifa ya Umoja wa Ulaya mjini Brussels kuhusu uhusiano na Urusi, ikwemo vikwazo kuhusiana na Ukraine, ambavyo vitahitaji kurefushwa tena mwishoni mwa mwaka huu.

Mkutano huo wa siku mbili mjini Brussels unatarajiwa pia kuzungumzia mchango wa Urusi katika kupambana na magaidi wanaoungwa mkono na Ulaya na Marekani nchini Syria, suala ambalo lilizusha mvutano wa hasira kati ya Urusi na Ufransa wiki iliyopita, na kumlaazimu Putin kufuta ziara yake mjini Paris baada ya serikali ya Ufaransa kupeleka mswada wa kutetea magaidi wa Syria katika baraza la Umoja wa mataifa.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky