Majeshi ya Saudia arabia yaendelea kuuwa raia wasio na hatia Yemen

  • Habari NO : 786628
  • Rejea : abna.ir
Brief

Majeshi ya Saudia arabia yameendelea kushambulia wananchi wa Yemen kwa kasi, katika kutekeleza azima yake ya kumrudisha madarakani kwa nguvu rais Mansur Haad ambaye wanachi hawamtaki.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Majeshi ya Saudia arabia yameendelea kushambulia wananchi wa Yemen kwa kasi, katika kutekeleza azima yake ya kumrudisha madarakani kwa nguvu rais Mansur Haad ambaye wanachi hawamtaki.

Mapigano yameendelea kushika kasi nchini Yemen leo hii ikiwa ni saa chache kabla ya kuanza kwa utekelezwaji wa mpango wa kusitisha mapigano kwa muda wa saa 72 katika nchi hiyo.

Kabla ya machafuko hayo mapya, serikali ya nchi hiyo ilikuwa imekubali mpango huo uliolenga kuruhusu misaada ya kibanaadamu kufika maeneo ambayo hayajafikiwa na misaada hiyo kwa miezi kadhaa. 

Duru za wakazi wa mji mkuu Sanaa zimeeleza kuwa kuongezeka kwa mapigano nchini Yemen, imetolewa wakati ambapo muungano wa majeshi unaoongozwa na Saudi Arabia, uliposhambulia kwa bomu makazi ya wananchi katika mji mkuu. Kumesikika vishindo vikubwa vya mabomu, baada ya mashambulizi mawili ya anga yaliyofanywa na ndege za muungano huo haramu dhidi ya eneo la makazi ya wananchi lililopo Mashariki mwa mji wa Sanaa na kupelekea watu kadhaa kuawa.

Haya yanakuja saa chache kabla ya kuanza kwa utekelezwaji wa mpango wa muda wa kusitisha mapigano kwa masaa 72, unaoanza jumatano hii. Taarifa iliyotolewa na Baraza tawala linalojumuisha wapiganaji wa kihouthi wanaoungwa mkono na Iran, na makundi ya kikabila yanayoshirikiana nao, imetaka muungano huo wa majeshi unaoungwa mkono na Saudi Arabia na Marekani kusimamisha mashambulizi ya kijeshi. 

Umoja wa Mataifa umesema mpango huo wa kusitisha mapigano kati ya mahasimu hao unatarajia kuanza saa sita kasoro dakika moja usiku wa jumatano hii kwa saa za Yemen, hatua inayoibua matumaini mapya ya kumalizika kwa vita hivyo vilivyosababisha vifo vya maelfu ya raia na kuacha wengine wakiteseka kwa njaa kali.

Baraza tawala la wahuthi na washirika wao  limetangaza kukubaliana na mpango huo wa kusititishwa kwa mapigano kwa kusema Yemen ilihitaji mpango wa haraka na endelevu bila ya kuwepo kwa masharti, ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa mzingiro kwa watu wa Yemen. 

Taasisi zinazotoa misaada ya kibinaadamu zitajaribu katika wakati huu wa kusitisha mapigani kuzifikia familia zilizoo kwenye maeneo ya miji na vijiji ambapo mapigano kati ya muungano wa mataifa ya kiarabu yakidhaminiwa na Marekani dhidi ya wananchi wa Yemen yalisababisha kuwepo kwa vikwazo va kusafiri na kusababisha raia wengi kukosa chakula na mahitaji mengine kama ya dawa.

Mratibu wa masuala ya kibanaadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen, Jamie McGoldrick amesema wana imani kwamba mpango huo wa kusitishwa kwa mapigano utawezesha taasisi zinazotoa misaada ya kibinaadamu kuyafikia maeneo ambayo haikuwa rahisi kufikiwa awali. 

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani ambaye nchi yake unaunga mkono Saudia arabia, John Kerry amesema, mpango huo uliotangazwa na Mjumbe maalamu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed, unahitaji kuwalazimu makundi hasimu kusitisha shughuli zote ze kijeshi ili kuwezesha kufikishwa kwa misaada.

Mwisho wa habari/ 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky