Mahmud Abasi: aliyefanya mauaji Yasir Arafat ninamfahamu

  • Habari NO : 791279
  • Rejea : ABNA
Brief

Rais wa Palestina amesema kuwa anajua chanzo cha kifo cha Yasir Arafat ambaye alikuwa ni kiongozi wa jumuia ya kuikomboa Palestina

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kiongozi wa Palestina Mahmud Abasi amesema kuwa anamfahamu kuwa nani aliyehusika na maua ya kiongozi wa zamani wa Palestina Yasir Arafat.
Mahmud Abasi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya miaka 12 ya kuwawa kwa kiongozi huyo wa Palestina, maadhimisho ambayo yalifanywa katika mji wa Ramadha nchini Palestina na kusisitiza kuwa: uchunguzi bado unaendelea wa kufuatilia mauaji ya Yasir Arafat bado unaenedelea, ama endapo mtu atauliza kuwa nani aliofanya mauaji ya kiongozi huyo, naweza kuwaambia kuwa nani alokuwa amehusika na mauaji hayo, lakini ushaidi wangu mimi pekee hautoshi kuthibitisha hilo, hivyo ni vyema kuendelea na uchunguzi alisema.
Uchunguzi bado ni wenye kuendelea na utakapo kamilika uchunguzi huo mtafikishiwa tija yake haraka iwezekanavyo, na hapo ndipo wote mtashikwa na butwaa kutokana na tija ya uchunguzi huo.
Yasir Arafat aliuwawa tarehe 11 mwezi November mwaka 2004 akiwa mwenye umri wa miaka 75, ambapo kifo chake kilitokea katika mji wa Paris nchini Ufaransa.
kwa mujibu wa maelezo ya mke wa marehemu ni kwaba marehemu alifariki baada ya kula aina ya madini ya Polonium, na mpaka sasa haijafahamika nani aliehusika na mauaji hayo dhidi ya kiongozi huyo.   
mwisho wa habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky