Papa atoaruhsa kwa maaskofu kusamehe waliotenda dhambi ya kutoa mimba

  • Habari NO : 793424
  • Rejea : abna.ir
Brief

Kwa kawaida katika dhidi ya kikristo ni maaskofu tu ama baadhi ya maaskofu wateule ambao wamepewa uwezo wa kusamehe dhambi za waumini wakosefu.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kiongozi wa Kanisa Katoliki leo ametoa moja kwa moja kifungu ambacho kinafanya kuwa rahisi kwa waumini wa kanisa Katoliki kuomba msamaha kwa dhambi kubwa ya kutoa mimba. Kifungu hicho maalum kilikuwa hapo kabla kikilenga kuwapo kwa muda tu wa jubilee ya msamaham, sherehe ya kikatoliki ambayo ilianza Novemba 8 , 2015 na kumalizika jana Jumapili.Katika kipindi cha Jubilee, ambacho pia kinafahamika kama mwaka mtakatifu, wanawake ambao walifanya utoaji mimba wanaweza kuomba msamaha kwa padre wa kikatoliki.

Kwa kawaida  katika dhidi ya kikristo ni maaskofu tu ama baadhi ya maaskofu wateule ambao wamepewa uwezo wa kusamehe dhambi za waumini wakosefu.

 Uamuzi huo ni mfano mwingine wa kuwapo tayari kwa papa Francis kukubali mabadiliko wakati inapokuja suala la sheria. Amewahi kusema kwamba anapendekea zaidi kukubali mabadiliko kuliko kung'ang'ania kanuni zisizopindika za kidini, msimamo ambao umemuweka katika mgongano na wahafidhina katika kanisa.

Mwisho wa habari/ 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky