Uturuki yatapatapa baada ya kutengwa na Umoja wa Ulaya

  • Habari NO : 795051
  • Rejea : abna.ir
Brief

Serikali ya Uturuki imedai kuwa haijafunga kitabu kuhusiana na Umoja wa Ulaya baada ya bunge la Ulaya kupendekeza kuzuia mazungumzo ya kujiunga nchi hiyo katika Umoja na kuitenga nchi hiyo wiki iliyopita,

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Serikali ya Uturuki imedai kuwa haijafunga kitabu kuhusiana na Umoja wa Ulaya baada ya bunge la Ulaya kupendekeza kuzuia mazungumzo ya kujiunga nchi hiyo katika Umoja na kuitenga nchi hiyo wiki iliyopita, rais Recep Tayyip Erdogan amesema leo, lakini ameongeza kwamba nchi hiyo ina mikakati mingine mbadala. Erdogan amesema wiki iliyopita kwamba Uturuki haikuhitaji kujiunga na Umoja wa Ulaya kwa gharama yoyote na imetafakari pia kuwa sehemu ya jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai , SCO, jumuiya ya kiusalama inayoongozwa na China, Urusi na mataifa ya Asia ya kati. Bila ya kueleza mikakati hiyo mbadala , Erdogan amesema leo kwamba mazungumzo na washirika wengine yanaendelea, akiuambia mkutano mjini Istanbul kwamba nchi hiyo inaweza kuendeleza hatua yake kuingia katika moja kati ya washirika hao wengine.

Uturuki ambayo imekuwa ndo njia kuu ya inayotumiwa na magaidi kuingia nchini Syria na Iraq na kutoa mali zinazoibiwa Syria na Iraq kupitia nchi hiyo imejikuta katika hali ngumu baada ya washirika wake wanaosaidiana na nchi hiyo kuwapa misaada magaidi nchini Syria na Iraq kuitenga nchi hiyo.

Kwasasa Uturuki inataka kujiunga na mataifa hasimu ya Umoja wa Ulaya na Marekani ambazo zimekuwa zikisaidiana na Uturuki katika njama kadha wa kadhaa dhidi ya Iraq na Syria, lakini wengi wahaamini kwamba Uturuki itakubaliwa kujiunga na jumuia ya SCO kutokana na tabia za kuwa na sura mbili na kigeugeu cha wanasiasa wa nchi hiyo.

Mwisho wa habari/ 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky