Rais wa Urusi amsifia Trump kuwa ni mtu mwenye upeo mkubwa

  • Habari NO : 796085
  • Rejea : abna.ir
Brief

Trump tofauti na raia Obama ambaye alijikitiza Zaidi katika kuchochea tofauti kati ya Marekani na Urusi na kusababisha hofu ya kupatikana vita vya tatu vya dunia.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Urusi Vladimir Putin amemsifu Rais mteule wa Marekani Donald Trump kuwa ni mtu mwenye upeo mkubwa na kutabiri kuwa atamudu kwa haraka majukumu yake mapya ikiwa ni pamoja na kutekeleza majukumu hayo kwa ufanisi. Rais Putin amekaririwa na shirika la habari la TASS kupitia mahojiano yaliyofanywa kati yake na kituo cha televisheni cha NTV kuwa Donald Trump anaonyesha kuwa na upeo mkubwa kutokana na mafanikio aliyoyapata katika biashara zake. Serikali ya Urusi ilisema mwezi uliopita kuwa viongozi hao wawili walikubaliana kurejesha mahusiano kati ya nchi hizo mbili katika hali ya kawaida pale walipozungumza kwa njia ya simu baada ya Trump kutangazwa mshindi wa urais wa Marekani katika uchaguzi uliofanyika mwezi Novemba. Alhamisi wiki hii Rais Putin alisisitza juu ya utayari wa nchi hiyo kushirikiana na utawala wa Trump pindi Rais huyo mteule atakapoanza rasmi majukumu yake ya uongozi mwezi Januari mwakani. Trump pia amekuwa akiusifu uongozi wa Rais Putin na kusema anatarajia kujenga mahusiano bora na Urusi.

Trump tofauti na raia Obama ambaye alijikitiza Zaidi katika kuchochea tofauti kati ya Marekani na Urusi na kusababisha hofu ya kupatikana vita vya tatu vya dunia.

Obama anaunga mkono upande wa magaidi nchini Syria ambapo Urusi inaunga mkono upande wa serikali, na huko Ukraine, Urusi inaunga mkono wapinzani lakini Marekani inaunga mkono upande wa serikali .

Mwisho wa habari/ 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky