Umoja wa Ulaya waitisha kikao kujadili ushindi wa majeshi ya Syria dhidi ya magaidi

  • Habari NO : 796979
  • Rejea : abna.ir
Brief

Umoja wa Ulaya ambao ni unaunga mkono upande wa magaidi nchini Syria, umelazimika kuitika kikao kujadili Ushindi wa jeshi la Syria ambao ni pigo kubwa kwa wadhamini wa magaidi nchini Syria ambao wamekuwa wakiwasaidia magaidi kwa zaidi ya miaka miatano.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Umoja wa Ulaya ambao ni unaunga mkono upande wa magaidi nchini Syria, umelazimika kuitika kikao kujadili Ushindi wa jeshi la Syria ambao ni pigo kubwa kwa wadhamini wa magaidi nchini Syria ambao wamekuwa wakiwasaidia magaidi kwa zaidi ya miaka miatano.

Wakati Ujerumani inakamilisha muhula wa mwaka mmoja kama mwenyekiti wa Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya-OSCE, Waziri wake wa Mambo ya Nje, Frank-Walter Steinmeier, ameitaka Urusi kushirikiana kikamilifu.

Wito huo ameutoa jana usiku kabla ya kuanza kwa mkutano wa siku mbili wa OSCE mjini Hamburg, Ujerumani, ambao unatarajiwa kutawaliwa na ajenda kuhusu Syria na Ukraine. Wakati wa mkutano wake na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov, siku moja kabla ya mkutano huo unaoanza leo, Steinmeier amesema Urusi inahitaji kusaidia kupunguza mivutano inayoongezeka barani Ulaya.

Ameitaka Urusi kutekeleza haraka mpango wa kusitisha mashambulizi dhidi ya magaidi nchini Syria ili kuruhusu magaidi hao kuondoka katika mji wa Allepo, kwa kisingizio cha kuruhusu misaada ya kibinaadamu kuingia nchini humo. Steinmeier amemtaka Lavrov kushinikiza kuwepo suluhisho la kisiasa katika mzozo wa Syria ulioanza mwaka 2011, Ombi hili la kutaka suluhisho la kisiasa linakuja baada ya magaidi wanaodhaminiwa na Umoja wa Ulaya ukishirikiana na Marekani wamezingirwa katika eneo dogo .

Karibu mawaziri 50 wa mambo ya nje pamoja na maafisa wa ngazi za juu wamekutana leo mjini Hamburg, katika Baraza la 23 la Mawaziri wa OSCE, huku ulinzi ukiwa umeimarishwa kwenye mji huo.

Polisi wamesema zaidi ya maafisa wa usalama 10,000 wamepelekwa mjini humo ili kuhakikisha usalama katika mkutano huo wa ngazi ya juu.

Urusi na mzozo wa Crimea

Kuhusu suala la Ukraine, Steinmeier ameikosoa Urusi kwa kuhusika katika mzozo wa mashariki mwa nchi hiyo, pamoja na kuitwaa Rasi ya Crimea mwaka 2014, baada ya rais wa Ukraine aliyekuwa akiungwa mkono na Urusi, Viktor Yanukovych kuondolewa madarakani. Aidha, ameitaka Urusi ihakikishe amani inarejea barani Ulaya. Amesema wanaamini kuwa baada ya kumalizika kwa Vita Baridi, suala la vita na amani linapaswa liwe limemalizika kabisa barani Ulaya, lakini bara hilo limekuwa katika migogoro ya mara kwa mara.

''Suala la vita na amani limerejea tena barani Ulaya, baada ya Urusi kujitwalia Crimea na mpaka sasa mchakato wa amani haujazaa matunda, licha ya kuwepo juhudi kadhaa za kumaliza mzozo huo. Na kwa sababu ya hilo, ni muhimu mataifa yote ya Ulaya yakaungana pamoja kwa ajili ya mazungumzo ya ana kwa ana yatakayosaidia kumaliza mizozo barani Ulaya na nje ya bara hilo, na sio tu kutoa matamko kupitia umma,'' amesema Steinmeier.

Muda mchache kabla ya kukutana na Steinmeier, Lavrov alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry na kuzungumzia mikakati ya kumaliza mapigano kwenye mji wa Aleppo, Syria. Kerry amewaambia waandishi wa habari mjini Hamburg, kwamba wamebadilishana mawazo kuhusu Aleppo na wanadhamiria kushirikiana ili kukomesha mapigano mjini humo.

Lavrov amesema amelikubali na kuthibitisha kuliunga mkono pendekezo la Marekani la ''Disemba 2'' linalotaka magaidi wa Syria kujiondoa kabisa kutoka mashariki mwa Aleppo. Hata hivyo, kuna uwezekano kwamba Urusi isifikie makubaliano yoyote hadi Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump atakapoingia madarakani. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watu 300,000 bado wamezingirwa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani ndani ya mji wa Aleppo.

Mwisho wa habari / 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky