Kwa gharama zozote tutakabiliana na uvamizi wa amani ya Taifa/ majeshi ya madui zetu yako ndani ya mitego ya majeshi ya Iran

  • Habari NO : 797374
  • Rejea : ABNA
Brief

Msaidizi wa majeshi ya Iran akizungumzia vitisho vya baadhi ya wanasiasa wa Marekani amebainisha kuwa: majeshi ya Iran hayana mzaha na yeyote katika kulinda mipka ya nchi, na endapo watakapo fanya jambo lolote linalopelekea uchafuzi wa amani ya taifa, watakutana na jawabu lisiowezekana kuelezewa

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na kamanda “Sayyed Masudi Jazairi” naibu wa majeshi ya Iran alipokuwa akitoa majibu ya baadhi ya vitisho vya baadhi ya wanasiasa wa Kimarerkani nakusisitiza kuwa: majeshi yetu hayana mzaha na mtu yeyote katika kuinlinda nchi hii, ambapo yeyote atakayejaribu kufanya hatua yeyote tishio kwa usalama wa taifa letu atakiona cha mtemakuni.
Aidha amesema: majeshi ya jamhuri ya kiislamu ya Iran hivi sasa ynasimamia kikamilifu Ghuba ya Uajemi, kuliko kipindi chochote kilichopita, kwa maana jeshi la sasa la jamhuri ya kiislamu ya Iran si kama la hapo kabla, hku akisisitiza kuwa wale wote waliokuwa na mpango wa kuzamisha mitumbwi ya kijeshi ya Iran, bila shaka hawajitambui kijeshi.
Kamanda huyo amesema: hali ya sasa ya kijeshi katika Ghuba ya Uajemi iko katika hali hii kwamba, majeshi na vifaa vya maadui zetu viko ndani ya mitego ya majeshi ya Iran.
Akitoa onyo kwa wapenda vita Marekani na vibaraka wake amesema kuwa: kama wapenda vita na mamluki wao, watapambana na cha mtemakuni kutoka kwa wapinganaji wa jeshi la Kiislamu.
Kamanda huyo alimazia kwa kubainisha kuwa: serikali ya Kiislamu ya Iran na majeshi yake, hayana mzaha na yeyote katika kulinda usalama wataifa lake, hivyo hatua yeyote itakayoonyesha kutaka kuvunja hali ya usalama na amni ya taifa bila shaka watapambana na chamoto.

mwisho wa habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky