Afisa usalama wa Uturuki amuua Balozi wa Urusi + Picha

  • Habari NO : 799387
  • Rejea : abna.ir
Brief

mtu aliyekuwa amebeba bastola ambaye anasadikiwa kuwa ni afisa uslama wa Uturuki alishambulia Balozi huyo kwa nyuma

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Andrey Karlov Balozi wa Urusi amepigwa risasi nchini Uturuki na kufariki.

Balozi huyo alishambuliwa katika eneo la sanaa ya uchoraji katika mji mkuu wa Ankara.

Ripoti zinasema kuwa balozi huyo alikuwa akitoa hotuba wakati mtu aliyekuwa amebeba bastola ambaye anasadikiwa kuwa ni afisa uslama wa Uturuki alishambulia Balozi huyo kwa nyuma na kutoa ujumbe kuhusu mji wa Aleppo nchini Syria.

Mji wa Allepo Syria ni ulikuwa ni ngome ya magaidi wanaoungwa mkono na serikali ya Uturuki, Marekani, NATO na umoja wa nchi za kisuuni za kiarabu, ambapo nchi hizo zinaunga mkono magaidi hao kwa lengo la kuangusha utawala wa kidemokrasia wa rais Bashar asad ambaye anaungwa mkono na Urusi na Iran.

Ushindi wa Majeshi ya Syria yanayosaidiwa na Urusi na Iran dhidi ya magaidi katika mji wa Allepo umekuwa ni pigo kubwa kwa Marekani, Ufaransa, Ujeruman, na washirika wao ambao wanaunga mkono upande wa magaidi nchini Syria.

Mpaka sasa serikali ya Urusi haijatoa tamko lolote kuhusu shambulizi hilo la kigaidi lililofanywa katika eneo lenye ulinzi wa hali ya juu karibu na ubalozi wa Marekani, katika mji mkuu wa Uturuki Ankara.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky