Serikali ya Urusi yakamata magaidi nchini humo

  • Habari NO : 801604
  • Rejea : abna.ir
Brief

Vyombo vya usalama vya Urusi vimewatia mbaroni watu saba wanaoshukiwa kupanga shambulizi la kigaidi mjini Moscow wakitekeleza amri ya kundi la kigaidi Daesh au Dola la Kiisilamu linalodhaminiwa na Saudia arabia ambalo linafanya jinai zake nchini Syria, Iraq, Nigeria, Yemen na Afghanstan.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Vyombo vya usalama vya Urusi vimewatia mbaroni watu saba wanaoshukiwa kupanga shambulizi la kigaidi mjini Moscow wakitekeleza amri ya kundi la kigaidi Daesh au Dola la Kiisilamu linalodhaminiwa na Saudia arabia ambalo linafanya jinai zake nchini Syria, Iraq, Nigeria, Yemen na Afghanstan. Shirika linalohusika na usalama wa ndani nchini Urusi ambalo pia linadhibiti matukio ya ugaidi nchini humo, FSB limesema leo kuwa maafisa wake wamewakamata washukiwa wa shambulizi hilo katika jimbo la Dagestan nchini humo. Wanamgambo wa makundi ya kigaidi katika jimbo la Dagestan wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya polisi na maafisa kadhaa na baadhi ya wanamgambo hao walionyesha kulitii kundi hilo la kigaidi linalodhaminiwa na Saudia arabia na washirika wkae. Urusi imekuwa ikishiriki mashambulizi ya anga dhidi ya magiadi wanaoungwa mkono na Marekani na saudia arabia nchini Syria tangu Septemba 2015 kwa lengo la kuisadia serikali ya Rais Bashar-al Assad na wananchi wa Syria. Rais Vladimir Putin pamoja na maafisa wengine nchini humo wanasema maelfu ya raia wa nchi hiyo na wengine kutoka mataifa yaliyokuwa yakiunda Jamhuri ya kisovieti wamejiunga na kundi la kigaidi la Daesh nchini Syria.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky