Urusi yatoa onyo kwa Marekani kuhusu vikwazo

  • Habari NO : 801606
  • Rejea : abna.ir
Brief

Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Urusi imesema iwapo Marekani itaiwekea vikwazo vipya nchi hiyo kufuatia madai ya Urusi kufanya udukuzi na kuingilia mchakato wa kampeni za uchaguzi ndani ya chama cha Democratic basi hatua hiyo itakua jaribio la kujaribu kuvuruga uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Urusi imesema iwapo Marekani itaiwekea vikwazo vipya nchi hiyo kufuatia madai ya Urusi kufanya udukuzi na kuingilia mchakato wa kampeni za uchaguzi ndani ya chama cha Democratic basi hatua hiyo itakua jaribio la kujaribu kuvuruga uhusiano kati ya mataifa hayo mawili. Kwa mujibu wa shirika la habari la RIA, serikali ya Rais Barack Obama inatarajiwa kutangaza hii leo hatua za kulipiza kisasi dhidi ya Urusi kutokana na kile kinachodaiwa Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani uliofanyika Novemba 8, mwaka huu na kumpa ushindi Donald Trump. Shirika la habari la RIA pia limeikariri wizara ya mambo ya nje ya Marekani ikisema vikwazo hivyo vipya vinaweza kubatilishwa na Rais Mteule Donald Trump wakati atakapokabidhiwa rasmi madaraka kutoka kwa Rais wa sasa Barack Obama.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky