Boko Haram yamkosoa raia wa Nigeria kwa kusema uongo

  • Habari NO : 801607
  • Rejea : abna.ir
Brief

Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau amezungumza kupitia picha ya video mpya akikanusha ripoti kwamba wanamgambo wa kundi lake, wametimuliwa toka kwenye ngome yao, katika msitu wa Sambisa.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau amezungumza kupitia picha ya video mpya akikanusha ripoti kwamba wanamgambo wa kundi lake, wametimuliwa toka kwenye ngome yao, katika msitu wa Sambisa. "Tuko salama. Hatukutimuliwa kutoka mahala kokote. Na mbinu na mikakati haitoweza kufichua wapi tuko kama Mungu hatoamua hivyo", amesema Shekau, katika video hiyo ya dakika 25, huku akiwa amezungukwa na wanamgambo walioficha nyuso zao. "Msiwaambie watu uwongo" amesema, akimtaja Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari aliyesema mnamo mkesha wa Krismasi kwamba wanamgambo wa kundi la kigaidi la Boko haram wameshindwa nguvu na kutimuliwa toka ngome yao ya mwisho msituni. Video hiyo imetolewa baada ya Rais Buhari kutangaza kwamba kampeni ya mwezi mzima ya kijeshi katika eneo hilo la msituni lenye kilomita 1,300 za mraba kaskazini mashariki ya jimbo la Borno imesababisha kuvunjwa nguvu moja kwa moja Boko Haram katika ngome yao ya msitu wa Sambisa.

Mwisho wa habari/ 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky