Wanane wakamatwa kwa tuhuma ya kuhusika katika tukio la kigaidi mjini Istambul

  • Habari NO : 802371
  • Rejea : ABNA
Brief

Watu wanane wakamatwa nchini Uturuki wakituhumiwa kuwa wamehusika katika kufanya tukio la kigaidi liliofanywa katika kiwanja cha mazoezi mjini Istambul

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: jeshi la polisi la Uturuki leo siku ya Jumatatu limewatia mbaloni watuhumiwa wanane wanaodaiwa kuhusika katika tukio la kigaidi nchini humo.
Watuhumiwa hao wanane wanadaiwa kuhusika kufanya shambulio la kigaidi katika sehemu za kufanya mazoezi katika nyakati za usiku. ambao inadaiwa kuwa watu hao walishiriki katika tukio hilo na hivi sasa wako china ya usimamizi wa polisi kwaajili ya uchunguzi zaidi.
Jeshi la polisi la Uturuki mpaka sasa halijatoa vielelezo na ushahidi wowote kuhusu watuhumiwa hao, huku wakibainisha kuwa watu hao ndio wakwanza kushikiliwa na polisi kuhusu tukio hilo liliofanyika katika jiji la Istambul Uturuki.
Kikundi cha kigaidi cha Daesh kilitangaza kuhusika na shambulio hilo liliofanyika katika viwanja vya michezo vinavyotumika nyakati za usiku katika mji wa Istambul, ambapo magaidi walikuwa wamefanya tukio hilo na kufanikiwa kutoroka katika sehemu ya tukio hilo.
Shambulio hilo lilitokea baada ya gaidi mmoja kuingia katika kiwanja cha michezo kinachotumika usiku na kuwafytulia risasi watu wote waliokuwa katika uanja huo, jambo ambalo limesababisha kuuwawa kwa watu 39 na na kujeruhiwa wengine 60 nchini humo.
Hivi sasa katika mji wa Istabul kumekuwa kukitokea mashambulizi ya kigaidi mara kwa mara, ambapo serikali ya Uturuki inadai kuwa matukio ya kigaidi yanayofanywa katika mji wa Istambul yanafanywa na kikundi cha kigaidi cha PKK na kikundi cha kigai cha Daesh.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky