Urusi yapunguza idadi ya wanajeshi wake Syria

  • Habari NO : 803226
  • Rejea : abna.ir
Brief

: Serikali ya Urusi imesema leo kuwa imeanza kupunguza idadi ya wanajeshi wake nchini Syria, chini ya masharti ya mpango wa kusitisha mapigano uliofikiwa kati ya makundi ya upinzani na serikali ya Syria, ambapo mpango huu waujahusu makundi ya kigaidi yanayodhaminiwa na Marekani na washirika wake.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Serikali ya Urusi imesema leo kuwa imeanza kupunguza idadi ya wanajeshi wake nchini Syria, chini ya masharti ya mpango wa kusitisha mapigano uliofikiwa kati ya makundi ya upinzani na serikali ya Syria, ambapo mpango huu waujahusu makundi ya kigaidi yanayodhaminiwa na Marekani na washirika wake.

Wakati hayo yakiarifiwa ndege za kivita za serikali ya Syria zimeyashambulia kwa mabomu wilaya muhimu inayoshikiliwa na magaidi wanaodhaminiwa na Marekani ambao walitia mafuta kwenye chanzo cha maji ya wananchi. 

Rais wa Urusi Vladmir Putin alitangaza kusitishwa kwa mapigano mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana na kusema kwamba nchi yake itayaondoa baadhi ya majeshi yake kutoka Syria , ambako majeshi yake  yakishirikiana na majeshi ya Iran yameisaidia Rais Bashar al-Assad na kuvunja njama za Marekani na washirika wake kutoka nchi 61 wenye mpango wa kuiangusha serikali ya Syria kama walivyofanya Libya.

Mkuu wa Jeshi la Urusi Valery Gerasimov amesema wameanza leo kuondosha manowari za kivita kutoka mashariki mwa bahari ya Mediterenia zinazoongozwa na meli ya kubebea ndege ya Admiral Kuznetsov. "Usitishaji mapigano katika maeneo yote ndani ya Syria kulianza tangu usiku wa Desemba 30 mwaka jana lakini hakuhusishi makundi ya kigaidi ya kimataifa na yale ya magaidi wanaodhaminiwa na Marekani. Kwa mujibu wa uamuzi wa Amiri jeshi mkuu Rais Vladimir Putin, wizara ya ulinzi inaanza kupunguza vikosi vyake nchini Syria."

Meli hiyo iliongoza kupelekwa kwa jeshi la majini la Urusi katika operesheni za pwani ya Syria, ikiwa ni nadra sana kuonekana tangu kuanguka kwa muungano wa kisovieti katika kutoa msaada kwa jeshi la Syria. Mashambulizi ya kiwango kikubwa dhidi ya vikosi vya magaidi wanaodhaminiwa na Marekani yalianzishwa kutoka katika manowari tangu mwezi Novemba.

Mkuu wa jeshi la Syria luteni Jenerali Ali Abdullah Ayoub ameitembelea meli hiyo kuhitimisha ujumbe wake. Katika hotuba yake iliyorushwa kupitia televisheni ya taifa ya Urusi, amesisitiza umuhimu wa usaidizi wa jeshi la Urusi kwa Damascus "katika vita dhidi ya ugaidi na hitaji la kuzidisha ushirikiano wa kijeshi" na Urusi hata baada ya "ushindi dhidi ya magaidi."

Wakati hayo yakijiri ndege za kivita za serikali nchini Syria zimeishambulia kwa mabomu wilaya inayodhibitiwa na magaidi wanaodhaminiwa na Marekani ambayo ni eneo kuu la chanzo cha maji baada ya magaidi hao kukata njia kuu ya usambazaji.

Damascus imekuwa bila maji kutoka Wadi Barada, tangu Desemba 22 na kuwaacha watu milioni 5.5 wakikosa huduma hiyo muhimu.

Umoja wa Mataifa ulionya hapo jana kwamba kuharibu vyanzo vya maji  ni uhalifu wa kivita.

Majeshi ya Urusi yamesema kuwa muda wowote yatarudisha meli zake za kivita kama yatahisi kuna hatari dhidi ya usalama wa wananchi wa Syria.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky