Askofu mkuu wa Urusi atangaza vita takatifu dhidi ya Daesh

  • Habari NO : 804030
  • Rejea : ABNA
Brief

Askofu mkuu wa Urusi atangaza vita ya kupambana na kikundi cha kigaidi cha Daesh akiisifu vita hiyo kuwa ni vita takatifu, huku akiyataka mataifa kupambana na kiota hicho cha shetani

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Askofu mkuu wa nchi ya Urusi ikiashiria hatari ya kikundi cha kigaidi cha Daesh, ametangaza rasmi vita nzito ya kukabiliana na kikundi hacho hatari na kuisifu vita hiyo kuwa ni vita takatifu.
Askofu huyo aliyasema hayo alipokuwa katika safari yake rasmi nchini Uingereza ya kuonana na viongozi wa nchi hiyo, akisisitiza kukabiliana na kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Kiongozi huyo wa wakristo amesisitiza katika maelezo yake kuwa: mataifa yote yanapaswa kushikamana katika kukabiliana na kikundi hicho hatari.
Aidha ameongea kusema kuwa katika vita hii wote wanapaswa kushiriki, haipaswi kuziacha nchi kadhaa zikipamana na zingine kukaa pembeni zikiangalia macho, hivyo wote wanapaswa kusimama dhidi ya kikundi hicho.
Askofu mkuu wa Urusi amesema; vita hii naipa jina lakuwa ni vita takatifu, ameyataka mataifa yote kushiriki katika vita hiyo.
Inasemekana kwamba serikali ya Urusi kwakushirikiana na Iran, Iraq na Syria inapambana vikali na vikundi vya kigaidi nchini Syria ikiwemo Daesh, ama mataifa ya nchi za kimagharibi pamoja yakuwa ilikuwa imeunda umoja wa kupambana na kikundi cha kigaidi cha Daesh lakini umoja huo unaonekana hauna mafanikio katika mapamano yake, hivyo inatakiwa kujipanga tena upya katika kufanikisha suala hilo hatimaye kukisambaratisha kikundi cha kigaidi cha Daesh katika uwepo wake.      
mwisho wa habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky