Rais Assad aapa kupambana na magaidi wanaozuia maji kwa wananchi

  • Habari NO : 804039
  • Rejea : abna.ir
Brief

Rais wa Syria Bashar al Assad ameapa kulikomboa eneo muhimu la usambazaji maji kwa mji wa Damascus ambalo linadhibitiwa na magaidi wanaoungwa mkono na serikali ya Obama.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Syria Bashar al Assad ameapa kulikomboa eneo muhimu la usambazaji maji kwa mji wa Damascus ambalo linadhibitiwa na magaidi wanaoungwa mkono na serikali ya Obama. Mamilioni ya watu wamekuwa wakiishi bila huduma ya maji kwa kipindi cha wiki kadhaa baada ya magaidi wanaoungwa mkono na serikali ya Obama kuharibu miundo mbinu katika eneo la Wadi Barada nje ya mji mkuu wa Syria, Damascus eneo ambalo ni muhimu katika usambazaji wa maji ya mji huo mkuu. Serikali inasema kwamba kundi ambalo zamani likifungamana na Alqaeda la Fateh al Sham Front ambalo lilijulikana awali kama Al Nusra Front liko katika mji huo wa Wadi Barada na inawalaumu magaidi wanaoungwa mkono na serikali ya Obama katika eneo hilo kwa kufunga maji yanayoelekea Damascus tangu Desemba 22. Vikosi vya Assad vimekuwa vikipambana katika mji huo wa Wadi Barada kwa wiki kadhaa sasa na mapigano yamekuwa yakiendelea licha ya kuanzishwa hatua ya kusitisha mapigano Desemba 30 katika nchi nzima. Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu milioni 5 wamekuwa wakiishi bila huduma ya maji mjini Damascus.

Mwisho wa habari/ 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky