Msaidizi wa Khalifa wa Daesh aangamia katika mji wa Musol

  • Habari NO : 804051
  • Rejea : ABNA
Brief

Msaidizi wa kiongozi mkuu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh “Abubakari Al-Baghdadi” ameangamia kufuatia shambulio la mabomu katika mji wa Musol nchini Iraq.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari za kuangamia kwa idadi kadhaa ya viongozi na makamanda wa kikundi cha kigaidi cha Daesh zimetangazwa nchini humo.
Makamanda watano wa kikundi cha kigaidi cha Daesh wameangamia akiwemo msaidi wa khalifa wa kikundi hicho “Abubakari Al-Baghdadi” kufuatia shambulio liliofnywa na majeshi ya Iraq katika kambi ya kikundi hicho katika mji Musol.
Moja kati vyanzo vya usalama nchi Iraq ametangaza kuwa; majeshi ya anga ya Iraq yakishirikiana na majeshi ya usalama wa nchi hiyo, wamefanya shambulio kali katika kambi ya “Al-Islahi Zirai” katika mji wa Musol nchini Iraq.
Katika shambulio liliofanywa katika kambi hiyo, imepelekea kuangamia makamanda watano wa kikundi cha kigaidi cha Daesh miunguni mwao ni “Abu Lui” ambaye ni msaidizi wa Khalifa wa kikundi hicho ambapo pia ni msimamizi wa masuala ya kilimo katika kikundi hicho.
Shambulio hilo limefanyika kwa umakini zaidi na majeshi ya anga ya Iraq baada ya kupata ripoti sahihi kutoka katika jeshi la usalama la nchi hiyo.
Mji wa Musol ni makao makuu ya serikali ya Khalifa wa Daesh nchini Iraq, Khalifa wa kikundi hicho Abubakari Al-Baghdadi alionekana siku moja katika msikiti mkuu wa mji huo na baada ya hapo hakuwa mwenye kuonekana tena katika mji huo.
Aidha mji wa Musol ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Iraq, mji ambao uko kaskazini mwa Iraq, ambapo mpaka sasa ni zaidi ya miaka miwili mji huo umetekwa na kikundi hicho cha kigaidi.
Mapambano ya kuukomboa mji wa Musol kutoka mikononi mwa Daesh yameanza toka miezi mitatu iliopita, ambapo majeshi ya Iraq mpaka sasa yamefanikiwa kukomboa maeneo mengi ya mji huo muhimu kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh.
mwisho wa habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky