Obama: vikwazo dhidi ya Iran vinaendelea

  • Habari NO : 805624
  • Rejea : ABNA
Brief

Rais wa jamhuri ya Marekani amebainisha kuwa: makubaliano yaliofanyika na Iran ni njia ya diplomasia iliotumika kuifanya Iran isiweze kutengeza silaha za nyuklia, ambapo makubaliano yaliofanyiaka ni njia bora zaidi kuliko kuiacha Iran itengeze silaha za nyuklia zisiokuwa na mipaka, au kutokea vita nyigine katika ukanda wa mashariki ya kati

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Rais wa marekani katika ujumbe wake kufuatia kukamilika kwa mwaka wa makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran, kwa mara nyingine tena imeituhumu jamhuri ya kiislamu ya Iran kuwa inasaidia vikundi vya kigaidi huku akisisitiza kuwa makubaliano ya nyuklia ya Iran ndio inayokubalika zaidi kuliko kuiacha Iran kuindelea na mpango wake wa nyuklia usiokuwa na mipaka.
“Baraka Obama” kwa mara nyingine ameituhumu Iran kwa kuvisaidia vikundi vya kigaidi na kusisitiza kuwa makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran ndio njia pekee iliokuwa inakubalika zaidi kuliko kuiacha Iran ikiendelea na mpango wake wa nyuklia usiokuwa na mipaka, au kupatikana vita nyingine katika ukanda wa mashariki ya  kati.
Aidha katika ujumbe huo ulio sambazwa katika mtandao wa ikulu ya marekani ameandika kuwa leo ni siku ya kumilika mwaka mmoja ya kupitishwa makubaliano ya pamoja ya mpango wa nyuklia wa Iran.
Naye amesisitiza kuwa makubaliano hayo yametoa tinja nzuri ya kuifanya Marekani na mataifa mengine dunia kupata amani na utulivu. Makubaliano hayo ya kihistoria waliokubaliana baina ya Marekani, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, China na Urusi ambapo makubaliano hayo yalikuwa yanamalengo ya kuizuia Iran isiweze kuifikia teknolojia ya nyuklia.
Aidha amesisitiza kuwa katika makubaliano hayo tulifanikiwa kuwekea mipaka mpango wa nyuklia ya Iran, ama kwakuwa Iran inaendelea kuvisaidia vikundi vya kigaidi dunia, vikwazo dhidi ya Iran bado vitaendelea.
mwisho wa habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky