Jengo la Plasco laporomoka mjini Teheran/ lauwa zimamoto 30+ picha

  • Habari NO : 805902
  • Rejea : ABNA
Brief

Jengo la Plasco liliopo mjini Teheran laporomoka na kwa masikitiko makubwa lasababisha vifo vya zimamoto 30 waliokuwa ndani ya jengo hilo ambapo kwaajili ya kuwaokowa wametekwa na moto ndani ya jengo hilo

Shirikala habari AhlulBayt (a.s) ABNA: jengo hlio awali ya yote lilianza kuungua katika tabaka za juu asubuhi ya leo na na baada ya kuathiri zaidi moto huo jengo likaporomoka, hivyo kufuatia kuporomoka kwa jengo hilo watu 30 miungoni mwa wafanyakazi wa zimamoto wamekufa ambao walikuwa wameingia katika jengo hilo kwaajili ya kuokoa waliopo katika jengo hilo kabla ya kuporomoka kwake.
Mkuu wa masuala ya maafa nchini Iran amesema kuwa mpaka sasa idadi kamili ya walioathirika katika tukio hilo bado haija fahamika, ama hospitali ziliokuwa karibu na sehemu hiyo ziko katika hali ya kupokea wathirika la tukio hilo, ama mpaka sasa watu 38 wameriptiwa kuwa wako katika hali ya matibabu.
Aidha ameashiria kuwa hivi sasa hofu tulionayo ni kuhusu waokozi wanaodhaniwa kuweko katika kifusi ambapo kipindi lilipokuwa jengo hilo linaporomoka walikuwa ndani wakiokoa watu katika uliokuwa unawaka katika matabaka ya juu ya jengo hilo.
Jengo la Plasco liko upande wa mashariki mwa midani ya Istambul katika mji wa Teheran, ambapo jengo hilo ni katika majengo ya awali yalikuwa na urefu wa tabaka 17 ambayo toka lijengwe mpaka sasa ni zaidi ya miaka 54 katika mji mkuu wa Iran Teheran.   


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky