Uturuki na Tanzania kusaini mikataba ya ushirikiano

  • Habari NO : 806879
  • Rejea : abna.ir
Brief

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan yuko nchini Tanzania kwa mazungumzo na Rais wa nchi hiyo John Pombe Magufuli na viongozi wengine wa nchi hiyo

Shirika la habari la ABNA linaripotikuwa: Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan yuko nchini Tanzania kwa mazungumzo na Rais wa nchi hiyo John Pombe Magufuli na viongozi wengine wa nchi hiyo katika ziara yake ya siku tatu mashariki mwa Afrika ambayo anatarajiwa kuweka msukumo kufungwa au kutaifishwa shule zinazomilikiwa na mhubiri wa kiisilamu Fethullah Gulen anayeishi nchini Marekani. Serikali ya Tanzania imesema marais hao wawili watasaini makubaliano katika maeneo saba ya ushirikiano. Kabla ya ziara hiyo Rais Erdogan alisema alipanga kuzungumza na viongozi wa Afrika kuhusiana na shughuli zinazofanywa chini ya mwamvuli wa Gulen barani humo. Uturuki inamtuhumu Gulen kwa kuhusika na jaribio la mapinduzi lililoshindwa mwezi Julai mwaka jana. Nchini Tanzania shule 11 zinazotumia jina la Feza chini ya mwamvuli wa Fethullah Gulen zina wanafunzi 3,000 zaidi ya nusu wakiwa ni waisilamu. Rais Erdogan anatarajiwa pia kuizuru Msumbiji na Madagascar.

Mwisho wa habari/ 291

 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky