Mfalme wa Jordan kufanya ziara Urusi kwa mazungumzo ya Syria

  • Habari NO : 807086
  • Rejea : abna.ir
Brief

Ikumbukwe kuwa Jordan ni moja kati ya nchi zenye mchango mkubwa katika kusababisha machafuko nchini Syria ambapo Majeshi ya Marekani yanatumia ardhi za Jordan, Uturuki na Qatar kuwapatia mafunzo ya kijeshi wapiganaji wa vikundi vya kigaidi nchini Syria.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mfalme wa Jordan Abdullah wa pili atafanya ziara mjini Moscow, Urusi kesho kwa mazungumzo na rais Vladimir Putin kuhusiana na mzozo wa Syria na mapambano dhidi ya ugaidi.

Taarifa kutoka kasri la mfalme zinasema viongozi hao wawili watajadili hali ya mambo katika mashariki ya kati, hususan mzozo wa Syria na hatua za amani kati ya Israel na Palestina. Waziri wa mambo ya kigeni Ayman Safadi pia anatarajiwa kukutana na waziri mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov mjini Moscow leo. Mkutano huo unakuja wakati serikali ya Syria na ujumbe wa waasi unafanya mazungumzo ya moja kwa moja ya amani nchini Kazakhstan, yaliyotayarishwa na Urusi na Iran zinazoiunga mkono serikali na Uturuki inayounga mkono baadhi ya makundi ya waasi.

Ikumbukwe kuwa Jordan ni moja kati ya nchi zenye mchango mkubwa katika kusababisha machafuko nchini Syria ambapo Majeshi ya Marekani yanatumia ardhi za Jordan, Uturuki na Qatar kuwapatia mafunzo ya kijeshi wapiganaji wa vikundi vya kigaidi nchini Syria.

Mwisho wa habari/ 291

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky