Rais mya wa Gambia aahidi kufanya mabadiliko katika

  • Habari NO : 807909
  • Rejea : abna.ir
Brief

Rais wa Gambia Adama Barrow ameahidi kufanya mabadiliko katika vikosi vya usalama nchini humo katika juhudi zake za kulijenga upya taifa hilo

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Gambia Adama Barrow ameahidi kufanya mabadiliko katika vikosi vya usalama nchini humo katika juhudi zake za kulijenga upya taifa hilo ambalo limekuwa chini ya utawala wa kimabavu kwa zaidi ya miaka 22 sasa. Katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu aingie rasmi madarakani alisema anatarajia kubadilisha jina la idara ya ujasusi nchini humo ambayo ilihusika kuwahoji na wakati mwingine kuwatesa watu waliotiwa mbaroni. Barrow ambaye alikula kiapo cha kuliongoza taifa hilo nchini Senegal alirejea Gambia Alhamisi wiki hii na kupokewa kwa shangwe na maelfu ya wananchi wa taifa hilo. Adama Barrow anakuwa Rais wa kwanza kuliongoza taifa hilo la Afrika magharibi baada ya kipindi cha zaidi ya miongo miwili chini ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh alielazimika kukimbiilia uhamishoni. Aidha amesema uchaguzi wa wabunge utafanyika April mwaka huu ikiwa ni moja ya hatua za mageuzi ya kidemokrasia nchini humo.

Mwisho wa habari/ 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky