Natanyahu abaki nje ya ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza akisubiri kuingia ndani + picha

  • Habari NO : 810146
  • Rejea : ABNA
Brief

Waziri mkuu wa serikali ya kivamizi ya Israel ambaye amesafiri kwenda nchini Uingereza kwaajili ya kuona na waziri mkuu wa nchi hiyo mjini London, Netanyahu kwakuwa alifika ofisi ya waziri mkuu mweza kabla ya muda uliopangwa, alibaki nje ya mlango wa ofisi ya waziri wa Uingereza haliyakuwa mlango wa ofisi hiyo ukiwa umefungwa

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: “Benjamin Netanyahu” waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel amewasili nchini Uingereza kwaajili ya kuonana na waziri mkuu wa nchi hiyo mjini Landon, ambapo Netanyahu aliwahi kufika katika ofisi ya waziri mkuu wa nchi hiyo na kulazimika kubaki nje ya ofisi kwa muda wa sekunde 15 hali yakuwa mlango mkuu wa jengo la ufisi ukiwa umefungwa mpaka ulipofika muda wa ahadi ndipo akafunguliwa mlango na kuingia ndani.
Netanyahu aliingia katika sehemu hiyo kinyume na ilivyo zoeleka kwamba hakuambata na waziri mkuu mwenza, jambo liliokuwa kinyume na ada ya viongozi wanapokufika katika ofisi hiyo.
Ama baada ya dakika mbili ya Netanyahu kuingia ndani, Theresa May “waziri mkuu wa Uingereza” alitoka nje akiwa na Netanyahu kwaajili ya kupiga picha ya pamoja nje ya jengo hilo nabaada ya hapo kuingia ndani.
Hii ikiwa ni mara ya kwanza kukutana baina ya mawaziri hao, toka baada ya kuingia madarakani kwa waziri mkuu mpya wa Uingereza “Theresa May” nchini humo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky