Magaidi 20 waangamia baada ya kichapo cha majeshi ya Iraq + Picha

  • Habari NO : 810338
  • Rejea : ABNA
Brief

Watu 20 miungoni mwa magaidi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh wameangamia kufuatia kichaapo kikali waliochokipata kupitia wapiganaji wa kujitolea katika jeshi la Iraq katika shambulio liliofanywa na jeshi hilo magharibi mwa Musol pia katika shambulio hilo magari matatu ya kijeshi yameangamizwa na majeshi ya Iraq

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wapiganaji wa kikundi cha Hashdu Shabiy wakishirikiana na jeshi la Polisi la Talafar wamefanikiwa kuwaangamiza magaidi 20 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh karibu na sehemu ya Al-hajaf kusini mwa Tel Abateh katika mji wa Musol nchini Iraq.
Miungoni mwa magaidi walioangamia katika sambulio hilo wako wanne kati yao ni magaidi maalumu wa kufanya mashambulio ya kujiripua ambao wameonekana wamevaa mikanda hiyo ya mabomu, pia majeshi ya Iraq yamefanikiwa kuangamiza magari mawili ya kivita katika shambulio hilo.


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky