Kiongozi wa kikundi cha Alqaida ameangamia nchini Syria + picha

  • Habari NO : 810536
  • Rejea : ABNA
Brief

Wizara ya ulinzi ya Marekani imetangaza kufa kwa magaidi 11 kutoka katika kikundi cha kigaidi Al-qaida ikiwemo mmoja kati ya viongozi wakuu wa kikundi hicho ambaye hapo mwanzo alikuwa pamoja na Osama bin Laden, mauaji hayo yametokea kufuatia shambulio la anga la Marekani karibu na mji wa Adlib nachini Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Pentagon imetangaza kuwa ndege za kijeshi za Marekani kufuatia mashambulizi ya mwezi huu yameangamiza magaidi 11 kutoka katika kikundi cha kigaidi cha Al-qaida, ikiwemo mmoja kati ya viongozi wa kikundi hicho ambaye alikuwa miungoni mwa watu wa karibu na Osama bin Laden, magaidi hao wamekufa karibu na mji wa Adlib nchini Syria.
Jeff Devis “msemaji wa Pentagon” amesema kuwa magaidi 10 wameuwawa katika shambulio la siku ya tarehe 3 mwezi huu, ambapo wengine wameuwawa katika shambulio la siku ya tarehe 4 mwezi huu ambapo pia aliuwawa (Abu Hani Almasriy) gaidi ambaye alikuwa karibu sana na kiongozi wa zamani wa kikundi hicho cha kigaid (Osama bin Laden).
Inasemekana kuwa gaidi huyo alikuwa anasimamia kambi za mafunzo ya kigaidi ya kikundi hicho mnamo mwaka 1980 na 1990 nchini Afghanistan, ambapo pia gaidi huyo alikuwa na fungamano la karibu na gaid (Ayman al-Zawahiri), ambapo baada ya kufa Osama mwaka 2011 alishika nafasi yake nakuwa kiongozi wa Al-Qaida.
   Jeff Devis alisema: mashambulio hayo yalifanywa kwaajili ya kupunguza nguvu ya kikundi hicho cha kigaidi itadhoofisha upangaji wa mashambulizi ya kigaidi katika mataifa mengine mashambulizi ambayo hutia dosari harakati za kiuchumi duniani.
Kuwepo kikundi cha kigaidi cha Al-qaida nchini Syria kimeingia kupitia kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusrah nchini Syria.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky