Kamanda wa kikundi cha Hizbullah Iraq katika mkoa wa Basra auwawa

  • Habari NO : 810541
  • Rejea : ABNA
Brief

Kamanda wa kikundi cha Hizbullah nchini Iraq katika mkoa wa Basra ambaye pia ni mmoja katika kamati ya mkoa huo ameuwawa na watu wasiofahamika nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: “Basim Al-musawiy” kamanda wa kikundi cha Hizbullah nchini Iraq katika mkoa wa Basra kusini mwa mkoa huo ameuwawa na watu walikuwa na silaha ambao mpaka sasa hawajafahamika.
Chanzo kimoja cha usalama katika mkoa wa Basra nchini Iraq ametangaza kuwa: Al-musawiy ambaye ni kamanda wa kikundi cha Hizbullah nchini Iraq katika mkoa wa Basra, ambaye pia ni katika wajumbe wa shura ya mkoa wa Basra ameuliwa na watu wasiofahamika huku watu aliokuwa nao kujeruhiwa vibaya.
Kamanda huyo alishambuliwa alipokuwa akipita sehemu ya al-Hayania katikati ya mkoa wa Basrah hatimaye kupoteza maisha baada ya tukio hilo.
Waliofanya mauaji hayo walipanda gari aina ya Pikap na kuifyatulia risasi gari iliokuwa imepanda kamanda huyo na kumpata risasi hizo katika sehemu ya kifua na tumbo, ambapo moja kwa moja alikimbizwa Hospitali na kuwekwa katika chumba maalumu kwaajili ya matibabu ama baada ya muda mchache alipoteza maisha kutokana na athari ya majaraha makubwa ya risasi hizo.
Vyombo vya ulinzi vya mkoa huo vimeanza kufanya uchunguzi na msako kwaajili ya kuwabaini waliohusika na tukio hilo la kigaidi.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky