Wanajeshi wa Uturuki wauwawa nchini Syria

  • Habari NO : 810579
  • Rejea : abna.ir
Brief

Wanajeshi watano wa Uturuki wameuwawa na 10 kujeruhiwa vibaya katika mapigano na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh wakati wanajeshi hao wakiwasaidia magaidi wanaopingana na Daesh katika operesheni ya kuuteka mji wa Syria wa al-bab

Shirika la habari la ABNA linaripo kuwa: Wanajeshi watano wa Uturuki wameuwawa na 10 kujeruhiwa vibaya  katika mapigano na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh wakati wanajeshi hao wakiwasaidia magaidi wanaopingana na Daesh katika operesheni ya kuuteka mji wa Syria wa al-bab kutoka kwa wapiganaji hao wa kundi la kigaidi la Daesh ambalo hapo kabla lilikuwa na uhusiano wa karibu na serikali ya Uturuki. Shirika la habari la Dogan limeripoti leo kwamba wanajeshi hao waliuwawa katika mapigano leo asubuhi na kifo chao kinafuatia kuuwawa kwa wanajeshi wengine watano wa Uturuki katika eneo hilo hilo hapo jana.

Wakati hayo yanajiri Shirika la misaada la kiarabu la Hilali nyekundu nchini Syria , linasema shambulio la kombora lililoreshwa na magaidi katika mji unaodhibitiwa na serikali wa Aleppo, limemuuwa mmoja wa watumishi wake wa kujitolea na raia wengine wawili ambao wakihitaji msaada. Shirika hilo linasema kombora liliangukia kwenye kituo cha usambazaji misaada katika eneo la Hamadaniya na kuwajeruhi watu wengine saba wafanyakazi wa Hilali nyekundu. Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limethibitisha tukio hilo. Majeshi ya serikali ya Syria yaliwashinda wapiganaji wa makundi ya kigaidi yanayodhaminiwa na Marekani katika mjini Aleppo mwezi Desemba baada ya miaka kadhaa ya mapigano makali, na kupelekea magaidi hao kukimbia mji huo huku Marekani na wadhamini wengine wa magaidi hao wakiilaumu Syria na Urusi kwa kufanya jinai za kivita.

Kushindwa kwa magaidi katika mji huo kulikuwa ni pigo kubwa kwa serikali ya Obama nan chi 61 zinazoshirikiana na Marekani katika kuwasaidia magaidi nchini Syria ili kuangusha serikali ya Bashar assad ambayo inaungwa mkono na Urusi, China na Iran.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky