Mogherini: makubaliano ya nyuklia ya Iran lazima yatekelezwe

  • Habari NO : 810793
  • Rejea : ABNA
Brief

Msimamizi mkuu wa siasa za mambo ya nje ya umoja wa Ulaya amesema: viongozi wa Marekani wamempa uhakika wa kutekelezwa kwa makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran ulifanyika kati ya Iran na nchi za 5+1

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: “Federica Mogherini” msimamizi wa siasa za mambo ya nje ya bara la Ulaya ameyasema hayo baada ya kuonana na “Michael Flynn” mshauri wa masuala ya usalama wa taifa la Marekani, ambapo Mogherini amesema: kufuatilia suala la utekelezaji wa makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran ni katika masuala  muhimu na nyenye kipau mbele katika umoja wa Ulaya.
Aidha ametangaza na kusema kuwa: Washington imetoa ahadi ya kuyatekeleza makubaliano ya mpango wa nyuklia yaliofanyika baina ya Iran na kikundi cha 5+1.
Msimamizi wa siasa za nje katika umoja wa Ulaya ametoa taarifa yakuwa amefanya mazungomzo na waziri wa mambo ya nje wa Marekani kuhusu utekelezaji wa makubalaino ya mpango wa nyuklia wa Iran.
Federica Mogherini akionyesha kufurahishwa kwake na kuonana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani na kuashiria kuwa baina ya Marekani na Umoja wa Ulaya kunafungamano la muda mrefu kati ya mabara hayo, huku akisisitiza kuwa kunamakubaliano mengi yapo mezani ambapo mpaka sasa hayajafanyiwa kazi, na endapo yatafanyiwa kazi faida yake zitarudi pande zote mbili.  
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky