Bomu la wataleban laua Watu 10 Pakistan

  • Habari NO : 811527
  • Rejea : abna.ir
Brief

Polisi nchini Pakistan wanasema bomu kubwa limelipuka katika mkutano wa hadhara katika mji wa Lahore mashariki mwa nchi hiyo na kuua watu wasiopungua 10.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Polisi nchini Pakistan wanasema bomu kubwa limelipuka katika mkutano wa hadhara katika mji wa Lahore mashariki mwa nchi hiyo na kuua watu wasiopungua 10. Miongoni mwa waliouawa ni maafisa wawili wa polisi wa cheo cha juu,akiwemo mkuu wa mkoa wa kitengo cha kupambana na ugaidi. Watu wengine 60 wamejeruhiwa katika mlipuko huo. Kwa mujibu wa maafisa wa polisi katika eneo hilo mlipuko umetokea wakati mwanamume aliyekuwa kwenye pikipiki aliugonga umati wa mamia ya wafamasia waliokuwa wakiandamana kupinga mageuzi mapya ya sheria ya uuzaji dawa. Kitengo cha kundi la Taliban kimedai kuhusika na shambulizi hilo.

Mwisho wa habari/ 291

 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky