Baraza la usalama kujadili makombora ya Korea Kaskazini

  • Habari NO : 811529
  • Rejea : abna.ir
Brief

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litakutana leo kujadili jaribio la kombora lililofanywa na Korea Kaskaszini. Kikao hicho kimeitishwa na Marekani, Japan na Korea Kusini kufuatia jaribio hilo

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litakutana leo kujadili jaribio la kombora lililofanywa na Korea Kaskaszini. Kikao hicho kimeitishwa na Marekani, Japan na Korea Kusini kufuatia jaribio hilo ambalo ni la kwanza tangu rais Donald Trump wa Marekani alipoingia madarakani. Baraza la usalama linatarajiwa kufanya mashauriano leo baada ya Korea Kaskazini kuthibitisha ilifaulu kufanya jaribio la kombora la masafa marefu lenye uwezo wa kuruka kilometa 10000. Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imesema kombora hilo liliruka umbali wa kiasi kilometa 500 kabla kuanguka baharini. Jaribio hilo linaonekana kama kipimo cha hatua itakayochukuliwa na rais Trump, ambaye ameahidi kuiunga mkono mshirika wake Japan asilimia mia moja. Korea Kaskazini imezuia chini ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa kutumia makombora yoyote ya masafa marefu na teknolojia ya nyuklia.

Hapo awali korea kaskazini ilifikia makubaliano  na kusaini mikataba ya Amani na Marekani, lakini Marekani ilienda kunyume na mikataba hiyo, na kuifanya Korea nayo kuvunja makubaliano hayo na kuendeleza kutengeneza makombora ya masafa Marefu.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky