Israel yakataa mazungumzo ya kujiondoa katika maeneo inayoyashikilia kwa nguvu+ Picha

  • Habari NO : 658253
  • Rejea : abna.ir
Brief

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekataa kuwa na mazungumzo juu ya kujiondoa kwa Israel mjini Jerusalem na katika Ukingo wa Magharibi kwa kipindi kisichozidi miaka miwili.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekataa kuwa na mazungumzo juu ya kujiondoa kwa Israel mjini Jerusalem na katika Ukingo wa Magharibi kwa kipindi kisichozidi miaka miwili. 

 Netanyahu ametowa kauli hiyo kabla ya kukutana na mwanadiplomasia mkuu wa Marekani John Kerry hapo kesho. Israel iliyateka maeneo ya Jerusalem, Gaza na Ukingo wa Magharibi wakati wa vita vya siku sita mwaka wa 1967 na kujiondoa mjini Gaza mwaka wa 2005. Netanyahu amesema kujiondoa katika maneno hayo kwa sasa kutasababisha wanamgambo walio na itikadi kali kuingia katika vitongoji vya Tel Aviv na hatimaye mjini Jerusalem. Akizungumza kabla ya  mkutano wa kila wiki wa baraza lake la mawaziri waziri mkuu hu-yo wa Israel amesema atalitaja suala hilo siku ya Jumatatu mjini Roma wakati atakapokutana na Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry, na Waziri Mkuu wa Italia Mateo Renzi. Wakati huo huo uongozi wa Palestina umepanga kuwasilisha rasimu ya azimio kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa kutaka Israel iache kuikalia kwa mabavu Palestina ifikapo Novemba mwaka 2016.

Israel inahistoria ya kuchukua kwa nguvu ardhi za nchi jirani ikiwemo Lebanon, Palestina, na Syria jambo linalopelekea wananchi wa Israel kutoishi kwa amani kwani wenye ardhi zao wameshatoa maonyo yakuzichukua kwa nguvu haki zao.

Leo kundi la Hamas limeonyesha silaha zake mpya na vifaa ya kisheji,ikiwa ni sherehe za kuazimisha miaka ishirini na saba tangu kuanzishwa kwa kikundi cha harakati za kimapinduzi cha wanamgambo wa Hamas. Msemaji wa kundi hilo Abu Ubaidah ameishukuru Jamhuri ya kiislamu ya Iran kwa kuisaidia misaada mbalimbali ikiwemo misaada ya madawa silaha na misaada mingine ya kibinadamu, pia amezishukuru Qatar na Uturuki kwa misaada  yake kwa wananchi wa ukanda wa Gaza.

Hizi ni picha za wanamgambo wa hamas wakiadhimisha miaka Ishirini na saba tangu kuasisiwa kwa kundi hilo linaloendesha vita dhidi ya Israel kwa ajili ya kurudisha aardhi zao zilizochukuliwa kwa nguvu na jeshi la serikali  ya Israel:


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky