Picha za Uvamizi wa mgahawa Sydney Australia

  • Habari NO : 658651
  • Rejea : abna.ir
Brief

Watekanyi nyara watatu wameuawa baada ya kikosi cha komando kuvamia eneo la tukio.
Watekaji nyara hao wameua watu wawili katika mgahawa huo.

Watekanyi nyara watatu wameuawa baada ya kikosi cha komando kuvamia eneo la tukio.

Watekaji nyara hao wameua watu wawili katika mgahawa huo.

Waziri Mkuu wa Australia, Tony Abbott, ameamuru bendera ya nchi hiyo kupepea nusu mlingoti, wakati taifa likiomboleza vifo vya watu wawili waliouawa kwenye mkasa wa kutekwa mgahawa katikati ya Sydney.

Licha ya watekanyi nyara wengine ambao ni raia wa nchi hiyo mmoja kati ya hao ni raia wa nchi hiyo mwenye asili ya Iran ambaye ametambulika kwa jina la Man Haron Monis

Monis alikuwa mmoja kati wa watu watatu waliouawa wakati vikosi vya usalama vilipouvamia mgahawa wa Lindt, katikati ya mji huo wa kibiashara. Kiasi cha wateja na wafanyakazi 17 walishikiliwa mateka kwa masaa 16 hapo jana, kabla ya kikosi maalum cha makamando kuuvamia mgahawa huo. Mmoja wa waliouawa ni meneja wa mkahawa huo, Tori Johnson, mwenye umri wa miaka 34, ambaye inaripotiwa kwamba alijaribu kumnyang'anya bunduki mteka nyara. Mwengine ni mwanasheria mwanamke, mama wa watoto watatu, Katrina Dawson, ambaye alikuwa akimkinga rafiki yake aliyekuwa mjamzito.

Wachunguzi wanasema kwamba wavamizi hao wanauhusiano na kundi la kigaidi la Daesh linalofanya jinai zake Syria na Iraq.


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky