Gavana wa Maryland atangaza hali ya hatari kufuatia mauaji ya Mmarekani mweusi + Picha

  • Habari NO : 686916
  • Rejea : abna.ir
Brief

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa serikali ya Marekani kukaa kimya, pindi wamarekani weusi wanapodhulumiwa au hata kuuawa, hali hii imepelekea raia wa Marekani wenye asili ya Afrika kuchukua sheria mkononi.

Gavana wa jimbo la Maryland nchini Marekani, Larry Hogan ametangaza hali ya hatari kutokana na ghasia zinazoendelea katika mji mkuu wa jimbo hilo Baltimore baada ya maziko ya Mmarekani mweusi Freddie Gray aliekufa kwenye mahabusu ya polisi.

Kwa mujibu wa taarifa, polisi wapatao 15 wamejeruhiwa, watu wamepora vitu madukani na magari kadhaa ya polisi yamepigwa moto. Tangu mwishoni mwa wiki iliyopita watu wamekuwa wanaandamana kupinga kifo cha Freddie Gray.

Gavana wa jimbo, Hogan pia ameliweka jeshi maalumu la taifa katika hali ya tahadhari. Amesema vitendo vya kupora mali na kutumia nguvu havitavumiliwa. Na mwanasheria mkuu wa Marekani Loretta Lynch amezilaani ghasia zilizozuka katika mji wa Baltimore na  amesema wizara ya sheria itatoa kila msaada utakaohitajika. Kwa mujibu wa habari, Freddie Gray aliekuwa na umri wa miaka 25 alikufa kutokana na uti wake wa mgongo kuumizwa vibaya sana.

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa serikali ya Marekani kukaa kimya, pindi wamarekani weusi wanapodhulumiwa au hata kuuawa, hali hii imepelekea raia wa Marekani wenye asili ya Afrika kuchukua sheria mkononi.


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky