Malaria

  • Habari NO : 249986

Malaria

Kwanza kabisa ni vyema tufahamu Malaria ni nini, husababishwa na nini,Mtu aliyepatwa na malaria huwa na dalili gani, matibabu na njia za kuuzuia .

Malaria ni ugonjwa unaoambukiza wanadamu wakati mbu aina ya Anopheles anapomuuma mtu. Mbu huyo wakati akimuuma mtu huacha vimelea vinavyojulikana kama plasmodium ndani ya mwili. Vimelea hivyo wakatii vikiwa ndani ya mwili, husafiri mpaka katika ini kupitia damu. Itafahamika kuwa mtu aliyeambukizwa vimelea vya malaria haugui mpaka vimelea vyote vya ugonjwa huo vitoke nje ya ini, ambapo huchukua muda wa wiki mbili tangu mtu aumwe na mbu.

DALILI ZA MALARIA NI ZIPI?

Dalili za awalii za malaria ambazo mara nyingi mtu huwa nazo ni hizi

zifuatazo: homa kali, kutetemeka mwili, kutokwa na jasho, maumivu ya kichwa na misuli, kuhisi kichefuchefu na kutapika. Lakini katika malaria kali inayosababishwa na kimelea hicho cha plasmodium falciparum mtu huwa na dalili zifuatazo: huonyesha hali ya kuchanganyikiwa, hupoteza fahamu, huwa na upungufu mkubwa wa damu na matatizo ya kupumua. Kwa hiyo kwa kutegemea dalili hizo tunaweza kujua iwapo mtu ameambukizwa malaria au la. Hata hivyo, ni vyema kwanza kumuona daktari baada ya kuona dalili za awali kama tulivyozitaja, ili aweze kukuandikia kipimo cha malaria.

Matibabu:

Kuna dawa mbalimbali za kutibu malaria (yaani Anti Malaria drugs) ambazo hutumiwa katika nchi zinazoathiriwa na malaria. Ni vyema kuashiria hapa kuwa, dawa za malaria zinaweza kubadilishwa mara kwa mara kwa kuzingatia mafanikio na athari inazotoa kwa mgonjwa. Kwa mfano nchini Kenya hivi sasa wanatumia dawa ya mseto ya Artemisinin, nchini Tanzania wameanza kutumia rasmi dawa ya Alu ambayo ni mchanyiko wa Artemether na Lumefantrine huku Uganda ikitumia dawa ya mseto ya ACT's. Hata hivyo, Daktari au mtaalamu wa afya ndiye anayepaswa kuainisha matumizi sahihi ya dawa hizo.

Tutajizuia vipi na Malaria?

Iwapo mtu anataka kusafiri kutoka eneo moja hadi jingine anashauriwa kwanza amuone daktari au muuguzi ili akushauri kuhusu dawa za kinga unazopaswa kutumia iwapo utashikwa na malaria huko uendako. Jambo la kuzingatia ni kuwa, ni lazima umalize dose yako ya dawa kama maagizo yanavyoeleza. Hakikisha unaelewa jinsi ya kunywa hiyo dawa kabla hujatoka katika ofisi ya daktari au muuguzi. Suala lingine muhimu la kuzingatia ni kuwa iwapo umegundulika kuwa na malaria wakati uko safarini unaweza kunywa dawa uliyoandikiwa, huku ukiendelea kutumia dawa yako uliyopewa kuzuia malaria.

Tutajizuiaje kuumwa na mbu

Kuna mambo mengi tunayoweza kuyafanya ili kuepuka kuumwa na mbu. Mbu huyo aina ya Anopheles anayesababisha ugonjwa wa malaria kwa kawaida huuma nyakati za usiku, lakini hata hivyo mbu wanaouma mchana nao wanaleta madhara mengi kwa mwanadamu, kwa hivyo nao wanapaswa kuepukwa.

Tufanye nini basi kujikinga na mbu:

1. Vaa nguo za kuzuia (yaani mashati ya mikono mirefu na suruali pamoja na nguo ndefu zinasaidia.

2. Tuwe na tabia ya kufunga madirisha mapema kabla ya kuingia giza na tuweke nyavu kwenye madirisha ya nyumba zetu.

3. Tutumie vyandarua katika kitanda wakati wa usiku kila inapowezekana. Ni vizuri zaidi kutumia chandarua kilichotiwa dawa ya kuulia wadudu ya ngao. Kwa mfano Tanzania na kenya baadhi ya watu hutumia vyandarua vya (NGAO).

4. Ni muhimu kujipaka dawa za kufukuza mbu. Dawa nzuri ya kufukuza mbu ni DEET yenye asilimia 25 hadi 50. Dawa za aina hizi hupatikana kwa wingi katika maduka mbalimbali. Unashauriwa kujipaka deet kila baada ya masaa 4 hadi 6 na zaidi kabla ya kwenda kulala. Ni salama kwa watoto na akina mama wajawazito, ila unatakiwa kuwa mwangalifu isiguse kwenye macho na midomo. Na dawa nyingine inayoweza kutumiwa ni ile ya DDT ambayo imeelezwa kuwa na mafanikio katika nchi za Afrika Kusini, Msumbiji na Nigeria katika kupambana na ugonjwa wa malaria.

5. Njia nyingine ya kuwaepuka mbu ni kuwa na tabia ya kusafisha mazingira yanayotuzunguka, kwa kukata majani marefu, kufukia vidimbwi vya maji vinavyowavutia mbu kuzaana kwa wingi na kadhalika. Muziki Muziki Muziki Muziki.

Hata kama ugonjwa wa malaria ni rahisi kutibika, lakini hivi sasa ni tishio kwa walimwengu. Takwimu za hivi karibuni za Umoja wa Mataifa zimethibitisha kuwa, watu milioni 300 hadi 500 huambukizwa maradhi ya malaria duniani kila mwaka, na kati ya idadi hiyo watu milioni moja hufariki dunia. Asilimia kubwa ikiwa ni watoto wachanga kutoka bara la Afrika. Kabla ya kukunja jamvi hili la makala hii yenye manufaa, leo nimewatayarishia dondoo moja muhimu ya kiafya. Je unafahamu tangawizi ina faida gani katika mwili wa mwanadamu?, Tegea sikio kwa makini mpenzi msikilizaji dondoo ifuatayo. Wataalamu wa afya wanasema kuwa mbali ya kuwa jamii zetu zimekuwa na mazoea ya kutumia tangawizi kama kiungo katika vyakula, lakini zao hilo linafanya kazi nyingi katika mwili wa mwanadamu kama vile kuimarisha tumbo, na kusaidia uyeyushaji wa chakula tumboni. Husaidia pia katika kutibu mafua ,rheumatism, kuhara na constipation au uyabisi wa choo, huondoa kichefuchefu na huzuia kutapika khususan kwa kina mama wajawazito, hupunguza maumivu ya tumbo, huondoa sumu mwilini n.k. Vile vile tangawizi ina wanga wa kutosha na haina mafuta. Aidha ina vitamini A,B1, B2, Madini ya Niacin, Sodium, Phosphorus, Potassium, Calcium, Iron au chuma, Maganesium, Coper na Zinc, ambayo yote yana faida kwa miili yetu.

 

 


Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky