Main Title
12 Februari 2025
Hatua za awali za kumaliza vita ya Ukraine na mustakabali usiojulikana
Baada ya Russia kumuachilia mfungwa Mmarekani, kitendo ambacho Rais wa Marekani alikielezea kama juhudi ya kumaliza vita vya Ukraine, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alitangaza kwamba yuko tayari kubadilishana ardhi na Russia.

12 Februari 2025
Mkuu wa Majeshi ya Oman: Mataifa ya ukanda huu ndio wamiliki wa eneo hili
Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Oman amesema kuwa: "Tutafanya kila tunaloweza kuhakikisha kunadumishwa ushirikiano katika eneo hilo, kwani mataifa ya ukanda huu ndio wamiliki wa eneo hili."

12 Februari 2025
Mpango wa Trump kwa ajili ya Gaza; njama za kuifuta Palestina
Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria upinzani mkubwa wa nchi za eneo na kimataifa dhidi ya mpango haramu wa Rais wa Marekani kuhusu Gaza na kueleza kwamba, mpango huo wa kuwahamisha kwa nguvu watu wa Palestina kutoka Gaza kwa mujibu wa mpango wa kikoloni wa "kuifuta Palestina".

12 Februari 2025
Kukimbia wanajeshi wa Marekani San'a ni ushindi mkubwa kwa Yemen
Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, kukimbia wanajeshi wanamaji wa Marekani mjini San'a ni ushindi mkubwa kwa wananchi wa Yemen na kusisitiza kuwa, kukimbia wanajeshi hao vamizi wa Marekani ni ishara ya kushindwa mradi wa kupenda kujitanua Washington nchini Yemen.

12 Februari 2025
Zaidi ya maghasibu 500,000 wa Kiyahudi wanaugua maradhi ya afya ya akili
Wazayuni milioni tatu wamekumbwa na matatizo ya kiakili baada ya Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa.

12 Februari 2025
Hamas yasisitiza: Watu wa Palestina watasalia imara katika ardhi yao
Harakati ya Mpambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imekariri upinzani wake dhidi ya matamshi yaliyotolewa Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu suala la kuwahamusha makazi Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza kwa kisingizio cha kulijenga upya eneo hilo.

12 Februari 2025
Tehran yalaani tishio la Trump la kutumia mabavu dhidi ya Iran
Iran imelaani vikali tishio la Rais wa Marekani, Donald Trump, la kutumia nguvu dhidi ya nchi hiyo na kusema linatia wasiwasi mkubwa na linaonyesha kutowajibika ipasavyo.

12 Februari 2025
Mkuu wa majeshi ya Iran: Umoja ndio njia pekee ya kukabiliana na utawala wa Kizayuni
Meja Jenerali Mohammad Bagheri Mkuu wa Majeshi ya Iran amesema kuwa, kwa kuzingatia dhati ya unyama na kupenda kujitanua utawala wa Kizayuni wa Israel, njia pekee ya kukabiliana na utawala huo vamizi na wa kigaidi ni mataifa ya eneo hili kudumisha umoja na mshikamano baina yao.

12 Februari 2025
Rais wa Iran apinga vikali mpango wa Trump wa kuwaondoa Wapalestina Ukanda wa Gaza
Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepinga mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kuwahamisha wakazi wa Gaza na kupelekwa katika nchi nyingine.

12 Februari 2025
Mahakama ya ICC: Tunalaani vikwazo vya Marekani kwa mwendesha mashtaka wetu
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) iliyoko The Hague huko Uholanzi imetoa taarifa ikilaani hatua ya utawala wa Donald Trump kumuwekea vikwazo Mwendesha Mashtaka wa mahakama hiyo, Karim Khan.

12 Februari 2025
Imam Khamenei: Wairani wamepuuza vitisho vya kijinga vya adui na kutuma ‘ujumbe wa umoja’ kwenye maadhimisho ya Bahman 22
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amelipongeza taifa la Iran kwa kufikisha "ujumbe wa umoja" kwa jamii ya kimataifa katika maadhimisho ya miaka 46 ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kihistoria ya Kiislamu ya Iran ya mwaka 1979.

11 Februari 2025
Independent: Chuki dhidi ya Waislamu nchini India zimeongezeka mnamo 2024
Ripoti iliyochapishwa na The Independent imefichua ongezeko kubwa la matamshi ya chuki dhidi ya Waislamu wa India na dini nyingine za waliowachache, na kumeripotiwa ongezeko la 75% katika 2024 ikilinganishwa na mwaka wa kabla yake.

11 Februari 2025
Papa: Mpango wa Trump wa kuwafukuza Wapalestina ni mgogoro mkubwa kwa Marekani
Papa Francis, kiongozi wa Wakatoliki duniani, ametaja kitendo cha utawala wa Trump kuwafukuza wahamiaji kuwa ni mgogoro mkubwa kwa Marekani.

11 Februari 2025
Ratiba ya wakati na mahali yatapofanyika mazishi ya Shahidi Nasrullah na Shahidi Safiyyuddin yatangazwa
Kamati ya vyombo vya habari inayohusika na shughuli ya mazishi ya Katibu Mkuu na Mkuu wa Baraza la Kisiasa la Hizbullah ya Lebanon waliouawa shahidi imetangaza kuwa shughuli ya mazishi hayo itafanyika siku ya Jumapili, Februari 19 saa saba mchana.

11 Februari 2025
HAMAS yasitisha mchakato wa kuwaachia mateka kutokana na Israel kukiuka makubaliano ya kusitisha vita
Brigedi za Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetangaza kuwa, zinasitisha mchakato wa kuwaachia huru mateka wa Israel uliopangwa kutekelezwa Jumamosi ijayo hadi litakapotolewa tangazo jengine, kutokana na utawala wa Kizayuni kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Ghaza.

11 Februari 2025
Hamas yapinga vikali kauli ya Trump, yanasema usitishaji mapigano ndio njia pekee ya kuwarudisha mateka wa Israel
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imelaani wito wa Rais wa Marekani wa kufutwa usitishaji vita katika eneo la Ukanda wa Gaza hadi pale harakati hiyo ya mapambano ya ukombozi wa Palestina itakapowaachia huru mateka wote wa Israel waliosalia katika muda wa siku chache, ikisema Donald Trump lazima akumbuke kwamba njia pekee ya kurejea mateka wa Israel ni kuheshimu mapatano hayo.

11 Februari 2025
Hizbullah ya Lebanon: Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalibadilisha sura ya historia
Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetoa salamu za kheri na baraka kwa taifa la Iran kwa mnasaba wa maadhimisho ya miaka 46 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ikisisitiza kuwa mapinduzi hayo yalibadilisha mkondo wa matukio na sura ya historia.

11 Februari 2025
Iran yamweleza Guterres: UN ichukue msimamo thabiti kuhusu njama ya Trump dhidi ya Palestina
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi amesema Umoja wa Mataifa, hasa Baraza lake la Usalama, lazima uchukue msimamo "imara na wa wazi" dhidi ya mpango wa Marekani na Israel unaolenga kuwaondoa kwa nguvu Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza.

11 Februari 2025
IRGC: Tutazindua karibuni kombora la 'supersonic cruise'
Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu karibuni hivi itazindua kombora la kisasa la cruise lenye uwezo wa kusafiri kwa mwendo kasi wa supersonic, lililotengenezwa na wataalamu wa humu nchini.

11 Februari 2025
Mwangwi wa maandamano ya Bahman 22 katika vyombo vya habari vya Marekani
Vyombo vya habari vya lugha ya Kiingereza vimeyapa kipaumbele maalumu maadhimisho ya miaka 46 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran yaliyofanyika jana kote nchini.
