Main Title
24 Septemba 2024
Sambamba na Lebanon, jeshi la Israel linaendelea kuteketeza roho za Wapalestina wa Ghaza
Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel linaendeleza mashambulizi na mauaji ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza mbali na vita vingine vya kinyama lilivyoanzisha dhidi ya Lebanon, ambako hadi sasa limeshaua watu wapatao 500, 100 miongoni mwao wakiwa ni wanawake na watoto.
24 Septemba 2024
Iran kurusha satelaiti 7 mpya katika anga za mbali
Mkuu wa Shirika la Anga za Mbali la Iran (ISA) amesema Jamhuri ya Kiislamu inapanga kutuma katika anga za mbali satelaiti tano hadi saba zilizotengenezwa ndani ya nchi. Operesheni hizo zitatekelezwa kabla ya kumalizika mwaka wa sasa wa kalenda ya Iran unaoishia tarehe 20 Machi 2025.
24 Septemba 2024
Rais wa Iran: Amani inapasa kuchukua nafasi ya vita duniani
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, amani na usalama vinapaswa kuchukua nafasi ya vita na umwagaji damu duniani. Rais Masoud Pezeshkian amesema hayo alipoona na wakurugenzi waandamizi wa vyombo vya habari vya Marekani mjini New York na kubainisha kwamba, Iran sio kama vyombo vya habari vya dunia vinavyoinyesha na tuko tayari kuishi kwa amani na usalama na dunia nzima.
24 Septemba 2024
Mohsen Rezai: Kisasi cha damu ya Ismail Haniyeh kinakuja
Mjumbe wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia jinai ya utawala wa Kizayuni ya kumuua kigaidi Ismail Haniyeh, Mkuu wa zamani wa Ofisi ya Kisiasa ya HAMAS hapa Tehran na kusisitiza kuwa, kisasi cha damu ya mwanamapambano huyo wa Palestina, kinakuja.
24 Septemba 2024
Rais Pezeshkian atilia mkazo kuimairishwa uhusiano wa kiusalama baina ya Iran na Uturuki
Rais Masoud Pezeshkian amefanya mazungumzo na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na kusisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuimarisha uhusiano wake wa pande zote na Uturuki yakiwemo masuala ya usalama.
24 Septemba 2024
Rais Pezeshkian: Iran haijawahi katu kuwa na nia ya kumiliki silaha za nyuklia
Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Iran amesema, Iran haijawahi katu kuwa na nia ya kumiliki silaha za nyuklia, bali imeheshimu na kutekeleza ahadi zake kulingana na makubaliano ya kimataifa ya JCPOA.
24 Septemba 2024
Akthari ya wananchi wa Marekani wanataka nchi yao irejee katika mapatano ya JCPOA
Watu wengi nchini Marekani wanataka Washington irudi katika Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA). Hii ni kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanyika huko Marekani.
24 Septemba 2024
Tathmini ya hotuba ya Rais wa Iran katika mkutano wa kuimarisha malengo ya Umoja wa Mataifa
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefafanua mitazamo ya Iran kuhusu 'Mkataba wa Mustakabali wa Kuimarisha Malengo ya Umoja wa Mataifa.
23 Septemba 2024
Kila saa moja linaripotiwa tukio la ubakaji katika mji mkuu wa Uingereza, London
Takwimu zilizotolewa na Polisi ya Uingereza zinaonyesha kuwa tukio moja la ubakaji huwa linaripotiwa kila saa katika mji mkuu wa nchi hiyo London.
23 Septemba 2024
UN yapitisha Mkataba wa Zama Zijazo (Pact for the Future), Guterres: Sasa ni wakati wa vitendo
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha Mkataba wa Zama Zijazo (Pact for the Future) baada ya vuta nikuvute zilizokuwepo ambapo Katibu Mkuu wa umoja huo Antonio Guterres ameshukuru wawezeshaji wote waliojitolea kufanikisha kupitishwa kwa mkataba huo adhimu.
23 Septemba 2024
Rais wa Colombia alaani kimya cha vyombo vya habari kwa mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel Ghaza
Rais Gustavo Petro wa Colombia amelaani kimya kinachoonyeshwa kwa vita vya kinyama vinavyoendelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza, na kusisitiza kwamba mauaji ya kimbari yanafanyika huko Palestina.
23 Septemba 2024
Erdogan: Tunasubiri jibu la Rais Assad kwa ombi la kurejesha uhusiano
Rais wa Uturuki amesema kuhusu mchakato wa kurejesha uhusiano kati ya Uturuki na Syria kwamba, tumesisitiza nia yetu ya kukutana na Rais Bashar al-Assad ili kuanzisha tena uhusiano wa uhusiano kati ya Ankara na Damascus.
23 Septemba 2024
Waziri Mkuu wa Lebanon atoa wito kwa jamii ya kimataifa kukabiliana na 'mauaji ya kutisha'
Waziri Mkuu wa Lebanon ametoa wito kwa jamiii ya kimataifa "kuchukua msimamo wa wazi" juu ya kile anachokiita "mauaji haya ya kutisha" katika taarifa iliyochapishwa jana.
23 Septemba 2024
Hizbullah yatwanga Haifa kwa kombora jipya la Fadi, wazayuni wengi waangamizwa
Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuwa imeshambulia kwa makombora kadhaa ya Fadi-1, Fadi-2 na maroketi ya Katyusha viwanda vya kijeshi vya Kampuni ya Rafael, ambayo inajishughulisha na vifaa vya kielektroniki, kaskazini mwa mji wa Haifa huko Israel.
23 Septemba 2024
Sheikh Naeem Qasim: Marekani ni mshirika wa jinai za utawala wa Kizayuni
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema Marekani ni mshirika wa mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza na Lebanon.
23 Septemba 2024
Jibu la awali la Hizbullah kwa chokochoko na uafriti wa Netanyahu
Baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kiongozi mwenyewe wa utawala huo bandia Netanyahu kukataa kusitisha vita katika Ukanda wa Ghaza na badala yake kuanzisha mauaji ya kigaidi kupitia hujuma za kimtandao nchini Lebanon, hatua hiyo sio tu imekwamisha juhudi za kurejeshwa amani katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na eneo kwa jumla,
23 Septemba 2024
Nabih Berri atahadharisha kuhusu hulka ya kupenda vita ya utawala wa Kizayuni katika eneo
Spika wa bunge la Lebanon ameashiria kuendelea mashambulizi ya utawala wa Kizayuni nchini humo na kusema, Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala huo anafanya kila awezalo ili kuitumbukiza Lebanon na eneo hili katika vita vikubwa.
23 Septemba 2024
Rais wa Iran asema undumakuwili wa nchi za Magharibi ni sababu kuu za vita, mauaji
Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amelaani misimamo ya undumakuwili ya nchi za Magharibi ambayo amesema imesababisha kuenea kwa umwagaji damu na vita duniani kote.
23 Septemba 2024
Kuongezeka kwa ukatili dhidi ya Waislamu Marekani
Bunge la Seneti la Marekani limefanya kikao kuchunguza ongezeko la uhalifu wa chuki katika nchi hiyo.
23 Septemba 2024
Nasser Kanani: Israel haitarejea katika kipindi cha kabla ya Kimbunga cha al Aqsa
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameutaja mlingano wa kistratijia katika eneo baada ya operesheni dhidi ya Uzayuni ya Kimbunga cha Al-Aqsa kuwa ulikuwa kwa manufaa ya Wapalestina na makundi ya muqawama. Amesema utawala wa Israel hautarejea katika hali uliyokuwa nayo kabla ya Kimbunga cha al Aqsa.