-
Moto mpya wa vita wawashwa na utawala wa Kizayuni huko Gaza kwa msaada wa Marekani
Kwa kukiuka makubaliano ya usitishaji vita huko Ghaza yaliyoanza kutekelezwa tarehe 19 Januari, utawala wa Kizayuni umeanzisha tena vita vya umwagaji damu dhidi ya eneo hilo lililoharibiwa na vita, kwa kufanya mashambulizi makubwa ya kinyama ambayo yamesababisha mauaji ya mamia ya mashahidi wa Kipalestina na kujeruhi wengine wengi katika ukanda huo.
-
Onyo la Iran kwa Marekani kuhusu matokeo mabaya ya uchokozi wa aina yoyote
Amir Saeed Irvani, Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa alitahadharisha katika barua yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu kwamba, hatua zozote za kichokozi zitakazofanywa na Marekani zitakuwa na matokeo mabaya na hatari mno.
-
Adhanom: Kukatwa misaada ya Marekani kunatishia maisha ya mamilioni ya watu
Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameonya kwamba kukatwa ufadhili wa Marekani kwa shirika hilo, mipango yake ya afya na mashirika mengine kunatishia uhai wa mamilioni ya watu.
-
"Jina langu ni Mahmoud Khalil, mimi ni mfungwa wa kisiasa"
Mahmoud Khalil, mwanafunzi wa Kipalestina katika Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani, amejieleza kama mfungwa wa kisiasa katika maoni yake ya kwanza tangu alipokamatwa na vyombo vya usalama vya Marekani kwa madai ya kuhusika katika maandamano ya watetezi wa Palestina.
-
Katibu Mkuu wa UN asema ameshtushwa na mashambulio mapya ya Israel Ghaza
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema, ameshtushwa na mashambulizi ya hivi karibuni ya anga yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza yaliyoua shahidi mamia ya Wapalestina wakiwemo watoto na wanawake.
-
Kwa nini Israel na Marekani zinaeneza chuki dhidi ya Uislamu kwa kutumia vibaya vyombo vya habari?
Utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani pamoja na baadhi ya nchi za Ulaya zimeendeleza vitendo vyao vya uharibifu na kuiondoa Televisheni ya Al-Aqsa katika satalaiti zote za kimataifa kwa lengo la kubana uhuru wa kujieleza.
-
Canada kuangalia upya mkataba wa kununua ndege za kivita za Marekani
Waziri Mkuu mpya wa Canada, Mark Carney ametoa amri ya kupitiwa upya mkataba wa nchi hiyo na kampuni ya silaha ya Marekani unaohusiana na kuiuzia Canada ndege za kivita za F-35.
-
Hatua ya Marekani ya kuishambulia kijeshi Yemen; kukariri mkakati ulioshindwa kufua dafu mbele ya Ansarullah
Donald Trump, ambaye aliingia madarakani kwa ahadi ya kuleta suluhu na amani na kuhitimisha vita kadhaa wa kadhaa vilivyoanzishwa na Marekani, ametoa amri ya kushambuliwa kijeshi Yemen baada ya kupita miezi miwili tu tangu ashike hatamu za utawala.
-
UN: Hatua za kimataifa zichukuliwe dhidi ya ongezeko la 'chuki dhidi ya Waislamu'
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameelezea wasiwasi wake juu ya "ongezeko la chuki dhidi ya Waislamu", akitoa wito kwa serikali kulinda uhuru wa kidini, na kwa majukwaa ya mtandaoni kuzuia matamshi ya chuki.
-
Utawala wa Trump kuwapiga marufuku au kuwawekea mpaka wa kuingia Marekani raia wa nchi 43
Gazeti la New York Times limeandika katika toleo lake la leo kuwa serikali ya Donald Trump inapitia mpango wa kuwapiga marufuku au kuwawekea mpaka wa kuingia Marekani raia wa nchi 43.
-
Utawala wa Trump wazidisha ukandamizaji dhidi ya wanafunzi wanaoitetea Palestina
Hatua ya serikali ya Marekani ya kumtia mbaroni mwanaharakati anayepinga vita na anayeunga mkono Palestina anayepata elimu nchini humo imezidisha wasiwasi kuhusu kushadidi makabiliano ya kiusalama na watetezi wa Wapalestina na vuguvugu la wanafunzi nchini Marekani.
-
Muirani afutwa kazi Marekani kwa kuwa AI imesema anaunga mkono Palestina
Chuo Kikuu cha Yale cha nchini Marekani kimemsimamisha kazi mhadhiri wa Kiirani kwa tuhuma zilizotegemea ripoti ya Akili Mnemba (Artificial Inteligence) ambayo imesema kuwa msomi huyo Muirani analiunga mkono taifa madhlumu la Palesitna hasa kutokana na kukosoa vikali mauaji ya kimbari yaliyofanywa na Israeli wakati wa vita vya Ghaza.
-
Maandamano dhidi ya Trump na Musk kila siku Washington DC
Mji mkuu wa Marekani, Washington DC, unaendelea kushuhudia maandamano ya karibu kila siku dhidi ya Rais Donald Trump kutokana na hatua zake za kuwaachisha kazi wafanyakazi, kubana matumizi na kusaini maagizo ya kiutendaji ambayo yanakiuka maslahi ya nchi.
-
Jamaatul-Islami yaitahadharisha serikali ya Pakistan isihadaiwe na hila za Trump
Mkuu wa Chama cha Kiislamu cha Jamaat-e-Islami Pakistan (JIP) ameihutubu serikali ya Islamabad akisema: Marekani si yenye kuitakia kheri katu Pakistan na haipasi kuridhia matakwa ya nchi hiyo.
-
Wacanada wenye hasira wamjibu kivitendo Donald Trump
sambamba na hatua ya rais wa Marekani, Donald Trump, ya kuongeza mashinikizo kwa Ottawa nwa vitisho vyake vya kuiteka Canada na kuijumuisha kwenye majimbo ya Marekani, wananchi wenye hasira wa Canada nao wameamua kutokaa kimya na wameanza kwa nguvu kutekeleza vikwazo dhidi ya bidhaa za Marekani.
-
UN: Utawala wa Trump uache kuingilia uhuru wa mahakama
Ripoti Maalumu wa Umoja wa Mataifa amekosoa vikali hatua za hivi majuzi za serikali ya Donald Trump ya kuwatimua na kuwateua maafisa wapya wa mahakama, akielezea wasiwasi wake kwamba hatua hizi ni sehemu ya vitisho kwa uhuru wa mfumo wa mahakama wa Marekani.
-
Wainjilisti wamshinikiza Trump kulipa wema, wamtaka aruhusu kunyakuliwa Ukingo wa Magharibi
Ripoti iliyochapishwa katika gazeti la Marekani, The New York Times, imefichua kwamba Wakristo wa Kiinjilisti, ambao walitoa huduma kubwa kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, wakati wa uchaguzi uliopita, ambapo karibu asilimia 80 walimpigia kura, sasa wanasubiri alipe fadhila na kuiruhusu Israel kutwaa Ukingo wa Magharibi, kwa madai ya ahadi ambayo eti Mungu aliwaahidi Wayahudi katika Biblia.
-
The Guardian: Trump anajifanya tu mbabe lakini ni mtu dhaifu
Gazerti la The Guardian la nchini Uingereza limeandika makala maalumu kuhusu misimamo dhaifu ya rais wa Marekani, Donald Trump katika masuala tofauti na kusema kuwa, ijapokuwa rais huyo anajifanya mbabe, lakini ni mtu dhaifu na vitisho vyake havina maana.
-
Trump na kukandamizwa uhuru wa kusema huko Marekani
Gazeti la Marekani la Washington Post limeandika makala likiashiria amri za utendaji zilizotolewa na Rais wa Marekani, Donald Trump, tangu aingie madarakani na kusema: Wakosoaji wanamtuhumu kuwa anakandamiza sana uhuru wa kujieleza na kukiuka Katiba ya Marekani.
-
Wacanada wenye hasira wamjibu kivitendo Donald Trump
sambamba na hatua ya rais wa Marekani, Donald Trump, ya kuongeza mashinikizo kwa Ottawa nwa vitisho vyake vya kuiteka Canada na kuijumuisha kwenye majimbo ya Marekani, wananchi wenye hasira wa Canada nao wameamua kutokaa kimya na wameanza kwa nguvu kutekeleza vikwazo dhidi ya bidhaa za Marekani.
-
Sasa Trump ameelewa, HAMAS haimuogopi
Mchambuzi mmoja mashuhuri wa ulimwengu wa Kiarabu amesema: "Kulazimika Donald Trump kuomba kufanya mazungumzo ni matokeo ya kufeli na kukata tamaa serikali yake katika njama zake za kuilazimisha Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS itii amri zake.
-
Onyo la Iran kwa Troika ya Ulaya kwa kukiuka Azimio la Umoja wa Mataifa na JCPOA
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa yaliyoko mjini Vienna, ametoa indhari kwa Troika ya Ulaya kuhusiana na ukiukaji wake wa Azimio la Umoja wa Mataifa na la Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA.
-
Wanachuo US walaani ukatili dhidi ya waandamanaji wanaounga mkono Palestina
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Columbia cha Marekani wamekosoa vikali jinsi uongozi wa chuo hicho unavyoshughulikia maandamano ya waungaji mkono wa Palestina, wakiushutumu uongozi huo kwa kusaliti jukumu lale na kuwadhaminia usalama wanafunzi na uhuru wao wa kujieleza.
-
Jaji wa Kijapani achaguliwa kuwa rais wa ICJ, atasimamia kesi ya mauaji ya kimbari ya Israel
Mahakama ya juu ya Umoja wa Mataifa imemchagua jaji wa Kijapani kuwa rais wake mpya, akichukua nafasi ya Nawaf Salam aliyeng’atuka madarakani Januari ili kuwa waziri mkuu wa Lebanon.
-
Trump: Wanafunzi wanaoshiriki maandamana ya kuunga mkono Palestina wataadhibiwa
Rais Donald Trump wa Marekani, ametishia kusitisha ufadhili wa serikali ya shirikisho kwa vyuo vikuu au taasisi zozote za elimu zinazoruhusu “maandamano haramu” kufanyika, akisema atachukua hatua kali dhidi ya wanafunzi wanaoshiriki maandamano hayo.
-
Jeshi la Israel latekeleza ‘Uvamiaji wa Kina Kabisa’ katika Ardhi ya Syria
Katika hali ya kuzidisha mgogoro kwa kiwango kikubwa, vikosi vya nchi kavu vya utawala haramu wa Israel vimefanya uvamizi wa "kina kabisa" hadi sasa katika eneo la Syria, vikilenga maeneo katika mikoa ya kusini-magharibi ya Quneitra na Dara’a.
-
Korea Kaskazini yalaani uchokozi wa kijeshi wa Marekani
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) imelaani vikali uchokozi wa kisiasa na kijeshi wa Marekani baada ya meli ya kubeba ndege za kivita ya Jeshi la Wanamaji la Marekani kutia nanga katika bandari ya Busan, Korea Kusini.
-
BBC yashinikizwa baada ya kufuta filamu kuhusu watoto wa Gaza
Watayarishi wa vipindi vya televisheni na filamu nchini Uingereza wamewataka wabunge wa Uingereza kuwahoji viongozi wa BBC kuhusu uamuzi wa shirika hilo la utangazaji la Uingereza kuondoa filamu ya kweli inayohusu maisha ya watoto Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
China yajibu mapigo dhidi ya ushuru mpya wa Trump
China imetangaza kujibu mapigo ya ushuru uliotangazwa dhidi ya nchi hiyo na Rais Donald Trump wa Marekani.
-
Misaada ya kijeshi na silaha ambayo haijawahi kutolewa mfano wake ya serikali ya Trump kwa utawala wa Kizayuni wa Israel
Sambamba na Marekani kukata misaada yake kwa Ukraine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, siku ya Jumapili alitumia mamlaka ya dharura aliyonayo kisheria kupitisha mpango wa utoaji msaada wa shehena ya silaha zenye thamani ya dola bilioni 4 kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.